Mbiringanya

Nondo Kishungi

Lymantriinae

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Uharibifu unao tokana na ulaji kwenye majani.
  • Kupukutika kwa majani wakati shambulio ni kali.
  • Uharibifu husababishwa na viwavi wa wadudu hawa.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mbiringanya

Dalili

Viwavi hutafuna majani, na kuifanya mimea kuonekana iliyo katwa katwa. Wanakula aina nyingi za mazao na miti. Idadi kubwa ya lava inaweza kusababisha mmea kukosa majani. Lava wanaweza pia kuguguna kidogo kidogo matunda machanga ambapo wanaweza kusababisha tunda kubadilika rangi na ngozi kuwa ngumu.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Bacillus thuringiensis inaweza kutumika kuwaondoa nondo kishungi, hasa wakiwa bado wachanga. Lakini huua tu viwavi wanaokula majani yaliyonyunyiziwa dawa na uwekaji wa pili unapendekezwa baada ya siku 7 hadi 10 kutokana na maisha yake mafupi baada ya kuwekwa. Spinosad pia ni nzuri lakini inaweza kudhuru nyuki na maadui wa asili. Ni sumu kwa nyuki kwa saa kadhaa baada ya kukauka. Spinosad haipaswi kutumiwa kwa mimea inayotoa maua.

Udhibiti wa Kemikali

Uvamizi wa nondo kishungi kawaida hudhibitiwa na maadui asilia, kwa hivyo kutumia viua wadudu kwa kawaida si lazima isipokuwa mimea ni michanga na ikaonyesha matatizo katika ukuaji. Ikiwa kuna uharibifu mkubwa wa majani, udhibiti wa kemikali unaweza kuwa suluhisho pekee. Ni muhimu kujua ni aina gani za dawa zinazoruhusiwa kwa matumizi haya katika eneo lako. Baadhi ya viambato amilifu ambavyo vimetajwa katika maandishi kwajili ya kudhibiti nondo kishungi ni pamoja na Chlorantraniliprole, Methoxyfenozide, na Phosmet. Kumbuka kwamba dawa za kunyunyuzia zinazotumiwa kudhibiti matatizo mengine ya viwavi wa majira ya kuchipua zinaweza pia kudhibiti nondo kishungi.

Ni nini kilisababisha?

Nondo Kishungi, hasa katika jamii/jinasi za Orgiia, Dasychira, na Euproctis, husababisha uharibifu kwa mimea duniani kote. Nondo waliokomaa wana nywele kwenye mwili wao wote na wanaweza kuwa kahawia, kijivu, au weupe. Nondo Kishungi hupitia hatua kadhaa katika mzunguko wa maisha yake. Nondo hutaga mayai kwa wingi katika msimu wa vuli, na mayai husalia kwa msimu wote wa baridi hadi msimu wa kuchipua unaofuata. Hali ya hewa inapokua ya joto, mayai huanguliwa na viwavi wachanga huibuka. Viwavi huanza kula majani ya mimea, miti na vichaka, hukua na kunyonyoka manyoya wakiendelea kula. Kadri wanavyokua, hujitengenezea kishada/ushungi wa manyoya mgongoni ambao humpa Nondo Kishungi/Kishada jina lake. Baada ya wiki chache za kula, viwavi wataunda kifuko/kiota. Ndani ya kifuko, kiwavi hubadilika na kuwa nondo kamili. Nondo waliokomaa hutoka kwenye kifuko na kujamiiana, na majike watataga mayai ili kuanza mzunguko upya. Idadi ya nondo huendelea kuongezeka katika maeneo ya karibu karibu kutokana na nondo majike kushindwa kuruka.


Hatua za Kuzuia

  • Ni muhimu kuwa makini unaposhughulika na nondo kishungi kwa sababu viwavi wake wana manyoya ambayo yanaweza kuwasha ngozi ya binadamu na kuchomoka kwa urahisi wakati akiguswa.
  • Vaa nguo za kujikinga na epuka kuvuta hewa yenye manyoya ya kiwavi.
  • Tafuta makundi ya mayai na viwavi wachanga na uwaondoe.
  • Ufuatiliaji wa wadudu daima ni njia bora zaidi.

Pakua Plantix