Riptortus pedestris
Mdudu
Wadudu hao huonekana wakiwa wamejikusanya kwenye maganda. Wana rangi ya kahawia au kijani mpauko. Wadudu wadogo na wakubwa hunyonya juisi ya mbegu zisizo komaa kutoka kwenye maganda ya kijani. Maganda yaliyoshambuliwa husinyaa na kuonyesha mabaka ya njano na makovu ya kahawia yenye mbegu ndogo. Ikiwa mashambulizi ni makali, sehemu laini za mmea zitasinyaa na hatimaye kukauka.
Kusanya kunguni/mende kwenye chombo chenye maji na mafuta ili kupunguza idadi yao. Wakati wa maua na uundaji wa maganda, mende wanaweza kukusanywa na kuuawa kwa mkono katika eneo dogo. Tumia mchanganyiko wa sabuni nyeusi na mafuta ya taa: Changanya 170 g ya sabuni nyeusi katika 150 ml za maji. Kisha weka mchanyiko huo katika lita 1 ya mafuta ya taa ili kuunda mchanganyiko mzito wa sabuni/mafuta ya taa. Weka 400 ml za mchanganyiko kwenye lita 5 za maji. Nyunyizia dawa kwa vipindi vya kila wiki baada ya kutokea kwa maganda.
Dimethoate, Methyl demeton, Imidacloprid au Thiamethoxam ni viua dudu muhimu na vyenye ufanisi ambavyo vinaweza kunyunyiziwa.
Mende wa ganda hupendelea siku za jua na viwango vya juu vya unyevu. Baada ya hali ya hewa kama hii, unaweza kuona uvamizi. Kunguni/mende wa kahawia nyeusi na mrefu mwembamba mwenye miguu mirefu. Mende/kunguni wadogo ni laini, wenye rangi ya njano-krimu na baadaye kugeuka kijani-kahawia. Kisha huanza kufanana na mchwa wa kahawia iliyokolea. Mende/kunguni wakubwa ni wa kahawia, wembamba na wapaa haraka na kuruka.