Njugu Mawe & Dengu Nyekundu

Mdudu Kudzu

Megacopta cribraria

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Wadudu wadogo, wa mviringo, wenye rangi ya kahawia nyepesi.
  • Majani kukauka.
  • Ukuaji usio wa kawaida wa maganda.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Njugu Mawe & Dengu Nyekundu

Dalili

Utaona wadudu wadogo, wa mviringo, wenye rangi ya kahawia na madoa meusi. Angalia kunguni wanaokusanyika kwenye mashina. Kula na kukusanyika kwa makundi makubwa kwenye mashina ya mmea. Kagua mimea kwa ukuaji usio wa kawaida wa ganda na madoa ya tishu zilizo kufa kwenye majani. Maganda hayakui vizuri na mbegu ni ndogo na nyepesi, na mbegu chache kwa kila ganda. Wadudu hao hufyonza virutubishi kutoka kwenye mimea: husababisha kukauka kwa majani na mashina. Madoa meusi yaliyo kufa kwenye mimea yanaonyesha mahali ambapo wadudu walikuwa wakitoboa na kunyonya virutubisho vya mmea. Wadudu walio komaa hula kwenye shina, wakati vizazi vichanga hula kwenye mishipa ya majani. Tambua harufu wanayotoa wanapovurugwa au kupondwa. Wadudu wa Kudzu huacha nyuma utomvu unao nata, wenye sukari kwenye majani. Kioevu hiki hulisha aina ya kuvu ambayo hutengeneza utando mweusi kwenye majani, kuzuia mwanga wa jua na hivyo kuzuia usanisinuru.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Beauveria bassiana ni fangasi ambao huathiri wadudu wa kudzu na husaidia kudhibiti mdudu huyu. Angalia ikiwa wanatokea kiasili: kunguni wa kudzu wa kahawia walio athiriwa watakuwa na utando mithili ya povu jeupe.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Usinyunyize dawa kwa wadudu walio komaa kwani haifai: hakikisha unanyunyizia vizazi vichanga. Nyunyiza pale tu utakapo ona wadudu waliokomaa 5 kwa kila mmea au zaidi mapema katika msimu. Acha wadudu walio komaa watulie na kunyunyizia vizazi vichanga wanapotoka kwenye mayai. Viua wadudu vinavyofaa ni pamoja na pyrethroids (β-cypermethrin, deltamethrin, sumicidin) na organophosphates. Imidacloprid pia imetumika kupunguza tukio la wadudu. Unyunyiziaji unao pendekezwa mwanzoni mwa uundaji wa maganda unaweza kudhibiti idadi ya wadudu na kupunguza idadi ya matumizi yanayo hitajika. Angalia kwa makini kabla ya kunyunyiza endapo Beauveria bassiana kuvu wenye manufaa wanaweza kuwa wanafanya kazi ili kupunguza idadi ya wadudu. Kuokoa muda na pesa zako!

Ni nini kilisababisha?

Kunguni hutumia majira ya baridi kwenye takataka za majani au chini ya gome la mti. Kunguni jike hutaga mayai yao marefu kwenye upande wa chini wa jani. Kizazi kipya kinachoanguliwa kutoka kwenye mayai haya kina umbo la mwili sawa na la wadudu walio komaa. Wanaanzia kwenye kingo za shamba na kuenea kuelekea ndani. Katika joto la chini na kupungua kwa urefu wa mchana, hujificha na kutumia majira ya baridi katika nyumba na huanza mzunguko mpya wa maisha katika mazao ya msimu ujao wa majira ya joto wenye joto zaidi.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina sugu ikiwa zinapatikana.
  • Wadudu huvutiwa na nyuso nyeupe: tumia mitego yenye kunata myeupe au manjano ili kuvutia na kunasa kunguni wa kudzu waliokomaa.
  • Ondoa mabaki ya mazao shambani mwako baada ya kuvuna.
  • Panda soya za msimu wa mapema kwenye mipaka ili kufanya kazi kama zao la mtego.

Pakua Plantix