Nezara viridula
Mdudu
Wadudu hula zaidi matunda na machipukizi yanayokua. Machipukizi yanayokua hukauka na kuanguka. Ulaji kwenye matunda husababisha uharibifu zaidi. Matunda hayawezi kukua kwa ukubwa unao stahili, kubadilika umbo na hata kudondoka. Mara nyingi, ulaji kwenye matunda husababisha madoa magumu meusi kwenye uso wa matunda. Ulaji kwenye machipukizi ya maua husababisha kudondoka kwa maua. Ladha ya matunda inaweza kuathiriwa. Maeneo yaliyo liwa huweza kuwa mahali pa kuingilia kwa vimelea na kusababisha uharibifu zaidi. Mayai mengi yanaweza kupatikana kwenye upande wa chini wa majani.
Vimelea wa mayai Trissolcus basalis na nzi wa tachinid Tachinus pennipes na Trichopoda pilipes wametumiwa kwa mafanikio kudhibiti mdudu huyu.
Uwekaji wa dawa kwa kawaida hauhitajiki/sio lazima, hata hivyo dawa za kunyunyuzia zinaweza kuhitajika ikiwa idadi ya wadudu wa kunuka ni kubwa. Mdudu huyu anaweza kudhibitiwa kwa kemikali kwa kutumia carbamates na misombo ya organophosphate. Hata hivyo, kiasi kikubwa cha misombo hii haidumu kwa muda mrefu sana kwenye mmea uliotibiwa, mazao yako katika hatari ya kuambukizwa tena kutoka maeneo ya karibu. Ufanisi wa udhibiti wa viua wadudu unaweza kuboreshwa kwa kuchukua fursa ya nyakati ambapo wadudu huwa hai na hawajajificha ndani ya majani. Kwa hiyo, dawa inaweza kuwafikia moja kwa moja. Mende wa kunuka huonekana wakila asubuhi mapema na alasiri.
Uharibifu huo husababishwa na mdudu anayeitwa Nezara viridula, ambaye hupatikana ulimwenguni kote, hasa katika maeneo ya tropiki na nusu-tropiki. Wanaitwa "mende wa kunuka" kwa sababu hutoa harufu kali wakati wanahisi kutishiwa. Wadudu hao hula kwa kutoboa mazao na sehemu zao nyembamba za mdomo za kutobolea (stylets). Tobo kutokana na ulaji halisi halionekani mara moja. Wadudu waliokomaa na wachanga wote hula mimea. Wanapendelea kula sehemu laini za mmea (machipukizi yanayokua, matunda, maua). Anapoangualiwa, hatua ya uchanga ya mende wa kunuka hukaa karibu na mayai. Wadudu waliokomaa wanaweza kuruka na kuzunguka sana. Kawaida ni wa kijani na kwa hiyo ni ngumu kuwatambua katika mimea. Rangi ya mdudu hubadilika kadri wanavyokua, na kuwa kijani kibichi kwa kila hatua. Kawaida huhamia sehemu za juu za mimea mapema asubuhi.