Mung'unye

Wadudu Mguu-jani

Coreidae

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Wadudu hawa wana miguu ya nyuma iliyo mithili ya jani.
  • Wadudu wenye miguu mithili ya jani husababisha ukuaji duni wa mazao.
  • Matunda kubadilika rangi sehemu ambapo wadudu wamekula.
  • Maeneo yaliyotitia/yaliyozama kwenye matunda.
  • Uharibifu kwenye majani na mashina.
  • Majani kubadilika rangi na kuwa ya njano au kahawia.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mung'unye

Dalili

Wadudu wa mguu jani wanaweza kusababisha dalili mbalimbali kwenye mazao, kutegemea na aina ya mdudu, hatua ya ukuaji, na aina ya mmea unaoathirika. Zifuatazo ni baadhi ya dalili za kawaida za uharibifu wa wadudu wa mguu jani kwenye mazao. Wadudu wa miguu jani wanaweza kusababisha ukuaji wa polepole wa mimea, hususani kwenye mimea michanga ambayo bado inayokua. Hali hii inaweza kusababisha mavuno madogo au ucheleweshaji wa kuvuna. Wadudu hawa pia wanaweza kusababisha mabadiliko ya rangi na matunda kuharibika umbo. Matunda yaliyoathirika yanaweza kuonekana kubadilika rangi, kuwa na umbo lisilo la kawaida au kuwa na maeneo madogo yaliyobonyea. Hali hii inafanya matunda kutokuwa na thamani sokoni kutokana na uharibifu huu unaoonekana. Wadudu wa miguu jani pia wanaweza kusababisha uharibifu kwenye majani na mashina ya mimea. Hali hii inaweza kusababisha majani kuwa ya njano au kahawia, kunyauka, na hata kufa kwa mmea. Zaidi ya hayo, baadhi ya aina za wadudu hawa zinaweza kusambaza magonjwa ya mimea ambayo yanaweza kuharibu zaidi mazao na kupunguza mavuno.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Sabuni za kuua wadudu au mimea, kama vile mafuta ya mwarobaini au pyrethrin (inayotokana na mawaridi ya jangwani), zinaweza kutoa udhibiti wa kiwango fulani kwa wadudu wachanga (yaani tunutu) pekee. Mojawapo ya njia bora za kudhibiti wadudu wenye miguu mithili ya majani ni kuondoa mayai yao.

Udhibiti wa Kemikali

Udhibiti wa kemikali kwa wadudu wa mguu-jani unahusisha kutumia dawa za kuua au kufukuza wadudu. Kuna aina kadhaa za dawa za kuua wadudu zenye ufanisi dhidi ya wadudu hawa, ikiwa ni pamoja na pyrethroids, neonicotinoids, na spinosad. Dawa hizi za kuua wadudu zinaweza kutumika kama za kupulizia, za unga unga, au chambo. Ni muhimu kufuata maelekezo kwenye lebo kwa makini unapokuwa unatumia dawa za kuua wadudu. Hakikisha unavaa mavazi na vifaa vya kujikinga, na epuka kupuliza dawa wakati hali ya hewa ni ya upepo au mvua. Pia, hakikisha unafuata makatazo yoyote yaliyoandikwa kwenye lebo kuhusu muda sahihi wa kutumia dawa husika na ni mara ngapi unaweza kutumia dawa hizo. Ingawa udhibiti kwa kutumia kemikali unaweza kuwa na ufanisi katika kupunguza idadi ya wadudu wenye miguu mithili ya majani, ni muhimu kutambua kwamba matumizi ya kupita kiasi au matumizi mabaya ya dawa za kuua wadudu yanaweza kuwa na athari mbaya, ikiwa ni pamoja na kwa wadudu wasiokusudiwa (ambao wengine wana manufaa), wanyamapori, na binadamu. Hivyo basi, ni muhimu kutumia dawa za kuua wadudu kwa uangalifu na iwe ni kama sehemu ya mbinu jumuishi ya udhibiti wa wadudu inayojumuisha udhibiti wa kitamaduni na wa kibiolojia.

Ni nini kilisababisha?

Wadudu wa mguu-jani ni wadudu amabao miguu yao ya nyuma ipo bapa ikiwa na umbile mithili ya majani. Ni wadudu wa ukubwa wa kati, mara nyingi wakiwa na urefu wa takriban milimeta 20, yaani sentimita 2. Mara nyingi wanakuwa ni wa rangi ya kahawia au kijani, na wanakula utomvu wa mimea, kama vile matunda, mboga, na mbegu jamii ya karanga. Mzunguko wa maisha wa wadudu hawa huanza wakati jike anapotaga mayai kwenye mimea. Urefu wa mayai ni takriban milimita 1.4, yana umbo la mduara, rangi ya shaba nyeusi hadi kahawia ya giza, na yanatagwa kwenye mistari. Mayai haya hutotoa tunutu wadogo (wadudu wachanga) ambao huonekana ni kama wadudu mguu-jani wadogo. Tunutu hupitia mabadiliko kadhaa kabla ya kuwa wadudu kamili. Katika kila hatua ya mabadiliko, tunutu huvua ngozi yake ya zamani na kuwa na ngozi mpya. Kadri wanavyokua, wananza kuonekana kama wadudu waliokomaa zaidi na kuanza kuwa na mbawa. Mara wadudu hawa wanapokuwa wamepevuka, huanza kupandana na kutaga mayai, na mzunguko wa maisha yao huanza tena. Wadudu wa mguu-jani wanaweza kupitia vizazi kadhaa kwa mwaka, kutegemea na hali ya hewa na upatikanaji wa chakula. Wanakuwa na uwezekano mkubwa wa kusababisha matatizo wakati mvua inaponyesha sana. Wadudu kamili (waliopevuka) hutoka mafichoni wakati wa majira ya kuchipua baada ya kutumia majira ya baridi wakiwa kwenye mimea iliyokufa au matandazo. Ikiwa majira ya baridi yana hali ya uvuguvugu, wadudu wengi zaidi watasalimika na kusababisha matatizo zaidi. Baadhi ya aina za wadudu wa mguu-jani huzaliana tu kwenye magugu, wakati wengine huzaliana kwenye mimea. Uharibifu wa matunda ndio jambo la kuhofia zaidi kutoka kwa wadudu hawa, na wana uwezekano mkubwa wa kusababisha matatizo wakati matunda yanapoanza kutokea.


Hatua za Kuzuia

  • Kagua mimea yako mara kwa mara ili kubaini dalili za pilikapilika za Mdudu Mguu-jani, kama vile mkusanyiko wa mayai, matunda yaliyobadilika rangi, maeneo yaliyotitia kwenye matunda, na uharibifu kwenye majani na mashina.
  • Unaweza kutumia vizuizi kama vile vifuniko vya mistari au nyavu/chandarua ili kuwazuia wadudu wa mguu jani kuifika mimea yako.
  • Ondoa magugu kwenye mashamba yako kwa sababu wadudu hawa wanaweza kujificha na kula magugu.
  • Hakikisha mashamba yako yanakuwa safi kwa kuondoa matunda yaliyodondoka au mabaki mengine yanayoweza kuvutia wadudu hawa.
  • Vutia au leta maadui wa asili wanaokula wadudu wengine (kwa mfano, ndege, buibui, na wadudu wanaokula wadudu wengine) ambao wanaweza kusaidia kudhibiti wadudu wenye miguu jani.
  • Unaweza kuvutia maadui hawa wa asili kwa kuwawekea makazi na maji.
  • Fanya usafi mzuri wa shamba lako mwishoni mwa msimu ili kupunguza uwezekano wa wadudu waharibifu kuishi hadi msimu unaofuata.

Pakua Plantix