Manduca sexta
Mdudu
Viwavi/minyoo hula majani machanga na mashina yanayo chipua, na kutengeneza matundu yanayo onekana na uharibifu wa nje ya majani. Ishara ya uwepo wao ni uchafu mweusi unao dondoka toka kwenye majani. Ukichunguza mmea kwa karibu, unaweza kuona viwavi/minyoo wa kijani au kahawia. Viwavi wanaweza kula majani yote kutoka kwenye mmea wa tumbaku, na kuacha tu shina na mishipa mikuu. Wakati wa milipuko mkubwa wa wadudu hao, mashamba yote yanaweza kuachwa yakiwa hayana majani kabisa. Kwa nyanya, mashambulizi makali yanaweza kusababisha viwavi kula matunda machanga yanayokua, na kuacha makovu makubwa yaliyo wazi kwenye matunda.
Tumia bidhaa za Bacillus thuringiensis (Bt) kulingana na lebo na miongozo ya ndani. Bt ni bakteria ambaye huua kiwavi endapo atamezwa, na ni salama kwa kilimo hai. Zaidi ya hao, wanyama asilia wanaokula wenzao kama ndege, mamalia wadogo, kunguni madoa na nyigu husaidia kupunguza idadi ya minyoo. Ikiwa utaona minyoo pembe ya tumbaku kwenye mimea yako, waondoe kwa mkono ukiwa umevaa glavu, na uwaweke kwenye ndoo ya maji ya sabuni ili kuwaua.
Kuna dawa kadhaa za kemikali kwa ajili ya kudhibiti minyoo pembe ya tumbaku na viwavi wengine. Malathion, diazinon, carbaryl, na fenitrothion ni dawa za kuulia wadudu ambazo hulenga hatua mbalimbali za ukuaji wa wadudu, lakini zinafaa hasa dhidi ya viwavi ambao tayari wanakula majani kikamilifu. Unapotumia dawa za kuua wadudu au bidhaa yoyote ya kemikali, ni muhimu kuvaa mavazi ya kujikinga, ikiwa ni pamoja na ulinzi wa macho, na kusoma kwa uangalifu maagizo ya lebo. Kanuni hutofautiana kulingana na nchi, kwa hivyo hakikisha unafuata miongozo mahususi ya eneo lako. Hii inahakikisha usalama na kuongeza nafasi za matumizi yenye ufanisi.
Dalili husababishwa na wadudu. Wadudu hawa hula tu kwenye mimea ya jami ya solanesi, kwa kawaida tumbaku na nyanya. Kiwavi/mnyoo anaweza kukua hadi kufikia urefu wa kidole cha shahada cha mtu mzima na ana "pembe" nyekundu au nyeusi mwishoni mwa mwili wake. Kiwavi kwa kawaida huwa na rangi ya kijani kibichi lakini pia anaweza kuwa na rangi ya kahawia na ana michirizi saba myeupe ya ulalo kila upande wa mwili wake na mboni ya macho ya bluu-nyeusi kila upande wa mwili wake. Nondo wa kike wa tumbaku hutaga mayai yake kwenye majani ya mmea mwenyeji. Kwa kawaida hawatagi mayai kwenye mimea ambayo viwavi/minyoo tayari wamekula. Yai huanguliwa na kiwavi hula majani na mashina ya mmea. Kiwavi hujivua ngozi yake mara kadhaa hadi wakati wa kupumzika, wakati ambapo kiwavi hubadilika na kuwa nondo aliyekomaa. Hatua ya kupumzika hupatikana chini ya ardhi au chini ya takataka za majani.