Embe

Kidugamba Mweupe wa Miembe

Aulacaspis tubercularis

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Majani kugeuka rangi kuwa ya njano, udondokaji wa majani, kukauka kwa matawi, uchanuaji hafifu wa maua, kudumaa kwa matunda na kuharibika umbile.
  • Kuanguka kwa matunda kabla ya wakati.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Embe

Dalili

Mimea hujeruhiwa kwa kunyonywa utomvu wa mimea kwenye majani, matawi na matunda. Chini ya uvamizi mkali wa wadudu, mimea ya miembe inaweza kubadilika rangi ya majani kuwa ya njano, kudondoka majani machanga, kukauka kwa matawi, na uchanuaji hafifu wa maua, na hivyo kusababisha ukuaji na maendeleo duni. Mabaka ya pinki yanaweza kuonekana kwenye ngozi ya nje ya matunda yaliyoiva ambayo hufanya mwonekano wa matunda usiovutia (uharibifu wa urembo), na hivyo kusababisha kupoteza thamani sokoni, hususani katika masoko ya kimataifa. Wingi wa wadudu hawa husababisha upotevu wa mavuno ya matunda kwa kiasi kikubwa.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Vidugamba weupe wa miembe wana maadui wengi wa kiasili. Wakulima wanaweza kutumia vivutio vya wadudu na virutubisho ili kuongeza idadi ya wadudu wanaowinda vidugamba weupe wa miembe kwenye mashamba. Inawezekana pia kuingiza maadui wa kiasili zaidi.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na tiba za kibaiyolojia, ikiwa zinapatikana. Tumia dawa za kuua wadudu zilizo chini ya udhibiti wa eneo lako na fanya mzunguko wa viambato hai vinavyotumika, ili kuepuka kutengeneza usugu wa wadudu dhidi ya dawa husika. Kumbuka kuwa matumizi ya madawa ya kupulizia majani ili kuua vidugamba weupe wa miembe zina ufanisi mdogo kwa sababu aina nyingi za miembe zinafika hadi urefu wa mita 20 na kwahiyo ni vigumu kwa vifaa vya kawaida vya kupulizia kuweza kufikia sehemu zote za mwembe, hususani juu.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na vidugamba weupe wa miembe, ambao ni wadudu wadogo wenye gamba gumu, wanaotokana na kundi la Hemiptera, familia ya Diaspididae. Wadudu hawa hushambulia mmea wa miembe katika hatua zote za ukuaji kutoka hatua ya kuwa mche hadi ukomavu. Wakati wa kula, wadudu hawa hufyonza utomvu na kuingiza sumu ndani ya mmea. Athari zake zinaweza kuwa kubwa zaidi wakati wa hali ya hewa ya joto na ukame kuliko wakati wa vipindi vya mvua, hususani kwenye miche michanga na miti ya miembe.


Hatua za Kuzuia

  • Chagua shamba linalofaa na aina bora ya mbegu.
  • Kwa mujibu wa tafiti kutoka Asia na Afrika, aina za maembe za Ataulfo, Apple, Haden, na Keit zimeripotiwa kuwa na uvumilivu zaidi dhidi ya kidugamba mweupe wa maembe ikilinganishwa na aina zingine kama Alphanso, Kent, Tommy Atkins na Dod.
  • Kagua vidugamba weupe kila baada ya wiki mbili na pogoa matawi yaliyoathirika ya miembe.
  • Hakikisha kunakuwa na nafasi ya kutosha ili mimea isishindane kwa sababu za ukuaji (kwa mfano, kushindania mwanga, chakula, n.k).
  • Kufunika matunda kabla ya kuvuna kunaweza kutumika kama njia ya ulinzi wa matunda(maembe).

Pakua Plantix