Zabibu

Vithiripi vya Mzabibu Mweusi

Retithrips syriacus

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Mabaka ya rangi ya fedha kwenye majani na matunda.
  • Madoa ya rangi ya kijivu na nyeusi inayong'aa kwenye majani (kinyesi cha wadudu).

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Zabibu

Dalili

Vithiripi hunyonya utomvu kutoka kwenye majani ya mmea wanamoishi, na kusababisha majani kunyauka na kudondoka. Mabaka yenye rangi ya fedha huonekana kutokana na kuingizwa mrija wa kithiripi kwenye jani. Katika maeneo ya kula, matunda hugeuka kuwa ya kijivu. Endapo uvamizi ni mkubwa, matunda huwa mabaya na hushindwa kukua kwa kawaida.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Tumia maadui wa kiasili kama vile wadudu walao wadudu wengine, mathalani wadudu-macho makubwa (Geocoris ochropterus) na utitiri/wadudu wawindaji (Metaseiulus occidentalis). Vithiripi wanaowinda,mbawakimia wa kijani, wadudu wa maua, na baadhi ya utitiri wa phytoseiid husaidia kudhibiti vithiripi wanaokula mimea.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia njia jumuishi zenye hatua za kukinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia, ikiwa yanapatikana. Vithiripi wanaweza kuwa vigumu kuwadhibiti kwa ufanisi kwa kutumia dawa za kuua wadudu, na kwa kiasi fulani, ni kutokana na uwezo wao wa kutembea, tabia yao ya ulaji, na hatua zilizolindwa za mayai na pupa (hatua za ukuaji wa wadudu zinazohusisha mabadiliko kamili yanayotokea kati ya hatua za lava na Vithiripi kamili). Dawa za kuua wadudu zinazotokana na spishi fulani za bakteria wa kwenye udongo (spinosad) zinachukuliwa kuwa zana za kudhibiti wadudu kwa njia ya kiasili. Kila wakati, fuata kanuni za kanda/eneo husika kuhusu usimamizi wa wadudu waharibifu.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na vithiripi kamili (waliokomaa) na lava (vithiripi wachanga) ambao hufyonza utomvu wa mmea. Vithiripi huanguliwa kutoka kwenye yai na hukua kupitia hatua mbili za lava wanaokula kwa nguvu.Vithiripi kamili majike wana urefu wa takriban milimita 1.4 hadi 1.5, na madume wana urefu wa milimita 1.3. Ni spishi yenye rangi ya weusi hadi kahawia nyeusi. Lava walioanguliwa huanza kula mara moja baada ya kuanguliwa, kawaida wakiwa katika makundi. Vithiripi kamili waliotoka karibuni (wapya) wana rangi nyepesi na nyekundu. Vithiripi hula upande wa chini wa jani lakini wakati uvamizi ni mkubwa, upande wa juu pia hushambuliwa, hususani wakati wa miezi ya baridi. Katika hali ya joto, mzunguko wa maisha kutoka yai hadi kuwa vithiripi kamili unaweza kukamilika kwa muda mfupi wa wiki 2.


Hatua za Kuzuia

  • Epuka kupanda mimea isiyostahimili mashambulizi ya magonjwa.
  • Fanya ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kufahamu uwepo wa vithiripi na kudhibiti magugu ya karibu ambayo huhifadhi vijidudu vya vithiripi.
  • Lima mimea inayoendana vizuri na hali za eneo hilo.
  • Hudumia shamba kwa mbinu sahihi za kilimo ili kuifanya mimea kuwa imara na kuiongeza uwezo wa kuvumilia uharibifu wa vithiripi.
  • Hakikisha mimea inamwagiliwa vizuri na epuka matumizi ya kupita kiasi ya mbolea ya naitrojeni, ambayo inaweza kuchochea ongezeko la idadi ya vithiripi.

Pakua Plantix