Mihogo

Usubi wa Vinundu wa Mihogo

Jatrophobia brasiliensis

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Kutokea kwa vinundu kwenye majani.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Mihogo

Mihogo

Dalili

Vinundu hutengenezwa kwenye mimea kutokana na lava kula majani. Vinundu hupatikana zaidi kwenye upande wa juu wa majani, ambako nzi hutaga mayai yao, na mara chache kwenye vichipukizi na mashina. Vinundu ni vya rangi ya kijani-manjano hadi nyekundu na vina umbo la koni. Wakati vinundu vinafunguka, vihandaki vyenye umbo la silinda vyenye lava au visivyokuwa na lava huonekana ndani ya vinundu. Endapo vinundu vinaonekana kutokea chini ya jani, tundu dogo huonekana, tundu ambamo usubi kamili hutokea.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Tumia mitego ya rangi kwa ajili ya ufuatiliaji au kuvuruga kujamiiana kwa wadudu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi kwa kuchukua hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaolojia yanayopatikana.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na nzi wa usubi waitwao Jatrophobia brasiliensis. Nzi hawa ni wadudu wadogo wanaoruka ambao hutaga mayai yao kwenye uso wa majani. Mayai yanapoanguliwa, lava wanaoibuka husababisha ukuaji usio wa kawaida wa seli, ambao hujitokeza kwenye sehemu ya juu ya jani.


Hatua za Kuzuia

  • Ikiwezekana, panda kwenye maeneo makavu.
  • Anzisha mashamba kwenye maeneo ya wazi na acha nafasi ya kutosha kati ya mmea na mmea ili kuruhusu uingizaji mzuri wa hewa.
  • Dhibiti magugu yaliyo chini na kuzunguka mimea.
  • Ondoa majani yote yaliyoanguka shambani na kisha yachome au yazike.

Pakua Plantix