Mbiringanya

Mbawakavu wa Maua

Oxycetonia versicolor

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Maua na vitumba vilivyoharibika.
  • Mimea iliyoshambuliwa sana inaweza kuonekana imechakaa kutokana na uharibifu unaotokana na kuliwa.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mbiringanya

Dalili

Mdudu huyu anaweza kusababisha upotevu mkubwa wa mavuno kutokana na uharibifu wa viungo vya uzazi. Mbawakavu waliokoma hula kwa ulafi maua na vitumba kwa kula chavua, chavulio na sehemu nyingine za uzazi ndani ya maua. Kwenye pamba, pia hushambulia vitumba laini. Aidha, mbawakavu hawa wameonekana wakitafuna vishina laini vya mimea ya biringanya na sehemu nyingine laini za tishu za mimea inayohifadhi wadudu hawa, hususani katika hatua ya uchanga.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hakuna matibabu ya kibaiolojia yanayojulikana kwa sasa.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kukinga pamoja na tiba za kibaiolojia, ikiwa zinapatikana. Hakuna matibabu ya kemikali yanayojulikana kwa sasa.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na mbawakavu wa maua waliokomaa. Mbawakavu wa maua ni mbawakavu warukao mchana na kimsingi ni wala chavua. Funza hukua kwenye Maada asilia (vitu vya kikaboni) kwenye udongo, na baadhi yao hushambulia mizizi, lakini bila kusababisha uharibifu mkubwa kwa mazao. Mbawakavu waliokomaa wana urefu wa milimita 7 - 15 na upana wa milimita 5 - 7. Jinsia zote mbili za mdudu huyu zinafanana. Mwili umejikusanya pamoja na kuwa na umbo la yai, na kwa kiasi fulani umbo bapa, akiwa na rangi angavu na mara nyingi rangi nyekundu ya kahawia na madoa/alama nyeusi na nyeupe.


Hatua za Kuzuia

  • Mbawakavu huyu huhama kutoka kwenye zao moja hadi lingine na ana wigo mpana wa mimea mbadala ya kuishi.
  • Kubadilisha mpangilio wa mazao na matumizi endelevu ya dawa za kuua wadudu kunaweza kumbadilisha mdudu huyu kutoka kuwa mdudu mdogo hadi kuwa mdudu mwenye hadhi ya juu.
  • Ufuatiliaji wa karibu na kuripoti kwa wakati juu ya mbawakavu huyu ni muhimu ili kuepuka mlipuko wowote kwa siku za usoni.
  • Kwenye mmea wa biringanya, matumizi ya dawa za kuua wadudu mara kwa mara dhidi ya vipekecha wa machipukizi na matunda husaidia kudhibiti idadi ya mbawakavu huyu.

Pakua Plantix