Mti wa jamii ya mchungwa

Vidugamba Theluji wa Michungwa

Unaspis citri

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Mkusanyiko mweupe wa magamba dume kwenye matunda.
  • Madoa ya njano upande wa chini wa majani.
  • Kuanguka mapema kwa majani.
  • Kukauka kwa matawi madogo.
  • Hatimaye, kufa kwa matawi.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mti wa jamii ya mchungwa

Dalili

Kwa kawaida mashambulizi hutokea kwenye shina na matawi makuu ya mti. Ikiwa mashabulizi kwenye hayo maeneo ya mti yanakuwa makubwa zaidi, basi matawi madogo, majani, na matunda pia huathirika. Hii husababisha madoa ya manjano kujitokeza upande wa chini wa majani, ambayo huanguka mapema, matawi madogo hukauka, na hatimaye kufa kwa matawi. Gome lililoathiriwa sana linakuwa jeusi na kudhoofika, linaonekana limekakamaa na hatimaye kupasuka, na hivyo kuruhusu kuvu kushambulia zaidi mti.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Nyigu wa vimelea vya Aphytis lingnanensis ni mzuri katika kusaidia kudhibiti Vidugamba Theluji wa Machungwa ikiwa tayari wamo ndani ya shamba. Tumia salfa ya chokaa (polysulfide sulfur) au salfa inayoweza kuchanganywa na maji, kisha acha angalau siku 30 kati ya kupulizia salfa ya chokaa na kupulizia mafuta. Hata hivyo, salfa ya chokaa inaweza kuathiri vibaya Aphytis lingnanensis ambao ni muhimu katika kudhibiti vidugamba. Mbawakawa/mbawakavu wa Chilocorus circumdatus pia ameonyesha kuwa wakala mfanisi wa udhibiti wa kibaiyolojia. Mafuta meupe, sabuni na dawa za kupulizia za mafuta ya mbogamboga hufanya kazi kwa kuziba mashimo ya kupumulia ya wadudu, na hivyo kukosesha hewa na hatimae kifo. Pulizia upande wa chini wa majani, mafuta ni lazima yaguse wadudu. Kupulizia sabuni au mafuta kwa mara ya pili inaweza kuwa muhimu baada ya wiki 3-4. Ufanisi wa vijidudu vya udhibiti wa kibaiyolojia unaweza kupungua kwa matumizi ya udhibiti wa kikemikali.

Udhibiti wa Kemikali

Wakati wote zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na tiba za kibaiyolojia ikiwa zinapatikana. Malathion 50% inafaa dhidi ya Vidugamba Theluji wa Machungwa, pulizia upande wa chini wa majani. Dawa za kuua wadudu za synthetic pyrethroid pia zinafaa dhidi ya viwavi hai. Hata hivyo, Malathion na synthetic pyrethroid zina uwezekano wa kuua maadui wa asili, kwa hiyo inapaswa kuepukwa ikiwa inawezekana.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na Vidugamba Theluji wa Machungwa waliokomaa (Unaspis citri). Yai la kidugamba theluji linakuwa na umbo la mviringo, lina rangi ya machungwa inayong'aa na urefu wa takriban 0.3 mm. Kidugamba jike aliyekomaa ana urefu wa 1.5 hadi 2.3 mm na magamba yao madogo, meusi mara nyingi hufananishwa kimakosa kwamba ni uchafu kwenye matunda. Majike huingiza sehemu zao za mdomo ndani ya mti na hawatoki tena, na hubaki wakila na kuzaliana hapo hapo. Ngao zao zina umbo mithili ya ganda la chaza, lenye rangi ya zambarau ya kahawia hadi nyeusi, na kingo ya kijivu. Magamba ya madume yenye ngao pia hayasogei hadi hatua ya kukomaa. Ngao za magamba ya madume ambazo hazijakomaa ni nyeupe zikiwa na pande zilizo sambamba na sehemu tatu zilizo wima, moja ikiwa katikati na mbili zikiwa ni zimeinuka pembeni. Vidugamba Theluji wa Machungwa hutoa kikoti cha kinga kilichotengenezwa kwa nta na ngozi zilizovuliwa na viwavi wadogo( wa hatua ya kwanza) wa awali, kikoti ambacho huunda ngao yao. Ngao itabaki kwenye matunda muda mrefu baada ya mdudu kufa, na kuharibu sura ya matunda.


Hatua za Kuzuia

  • Safisha vifaa vya kilimo kabla ya kuhamia kwenye miti/mashamba mapya.
  • Piga brashi mavazi yako kabla ya kuingia eneo jipya la shamba.
  • Tunutu wanaweza kuhamishwa na upepo, vifaa vya kilimo, na wafanyakazi shambani.
  • Kwa kuwa tunutuwa Kidugamba Theluji wa Machungwa ndio hatua ya kutembea, kuzuia usambaaji wa hatua hii ni muhimu.

Pakua Plantix