Leucoptera sp.
Mdudu
Mwanzoni, mitaro/mashimo yanatengenezwa na baadaye yanaenea kwenye eneo kubwa, na kusababisha mabaka makubwa yanayotokana na kufa kwa tishu za majani. Viwavi wapo ndani ya mashimo na hula mesofili(tishu za ndani ya jani). Majani yanaharibika na usanisinuru hauwezi kufanyika. Mimea hupoteza majani na hatimaye hufa.
Mbinu za usimamizi wa mazao na muundo wa mandhari zinaweza kuathiri jamii za wadudu na huduma za mfumo wa ikolojia zinazotolewa na maadui asilia, na hivyo kuongeza utofauti na wingi wao. Mifumo changamani kiikolojia ya kahawa inahusishwa na bioanuwai kubwa ya vimelea vya nyigu, siafu, na wadudu wanaowinda na kula wadudu wengine. Hata hivyo, hakuna juhudi kubwa iliyofanywa ya kutumia maadui hawa asilia kama njia ya udhibiti wa kibayolojia. Mitego ya harufu inaweza kutumika kudhibiti au kuvuruga tabia za asili za wadudu ili kupunguza idadi yao.
Daima zingatia mbinu jumuishi pamoja na hatua za kuzuia na matibabu ya kibayolojia yanayopatikana. Hivi sasa, wakulima wa kahawa hutumia dawa za kuua wadudu za neurotoxic, kama vile organophosphates, carbamates, pyrethroids, neonicotinoids, na diamides. Hata hivyo, udhibiti wa kikemikali hautoshi na unaweza kupoteza ufanisi wake kwa sababu matumizi yake yanaweza kusababisha wadudu kuwa sugu.
Uharibifu husababishwa na lava wa Kidomozi wa Kahawa, ambao hula majani ya kahawa pekee. Vidomozi kamili (waliokomaa) hupandana usiku na majike hutaga mayai yao juu ya majani ya kahawa. Muda wa kabla ya utagaji wa yai la kwanza (muda wa tangu kutokea kwa kidomozi kamili hadi kutaga yai lake la kwanza) ni siku 3.6 katika joto la 20°C. Kwa wastani, kila yai lina ukubwa wa takribani milimita 0.3 na ni vigumu kuyaona kwa macho bila kutumia hadubini. Wakati wa kuanguliwa, viwavi hutoka upande wa chini wa mayai ambayo yanagusana na epidemisi (tabaka la seli) ya juu ya jani na hupenya ndani ya jani. Viwavi ni ang'avu na hufikia urefu wa milimita 3.5. Viwavi hula mesofili (tishu za ndani ya jani) ya majani na kutengeneza mitaro kwenye majani. Mitaro hiyo husababisha kufa kwa seli za jani, kupunguza eneo la jani kwa ajili ya usanisinuru. Hii husababisha kiwango cha chini cha usanisinuru wa mimea na hivyo kusababisha mmea kufa kabisa. Hatua ya viwavi ina awamu nne za mageuzi. Lava huiacha mitaro na kufuma kifuko chenye umbo X kwa uzi wa hariri, kwa kawaida katika eneo la kwapajani, na kuunda pupa. Kwa kawaida, pupa wengi hupatikana upande wa chini wa mmea ambako majani mengi yaliyokufa hukusanyika. Kutoka kwenye hatua ya pupa, wadudu kamili hutokea wakiwa na wastani wa urefu wa mwili wa milimita 2 na upana wa mbawa wa milimita 6.5. Wana magamba ya nywele nyeupe na antena ndefu zinazofikia mwisho wa tumbo na mbawa za rangi ya kahawia-nyeupe na zenye nyuzi nyuzi. Wakati wa kutoka wadudu kamili kutoka kwenye hatua ya pupa, hupandana na kutaga mayai, na hivyo kuanza tena mzunguko wa maisha. Kuenea kwa mdudu huyu kunasaidiwa zaidi na msimu wa ukame na joto kali.