Muwa

Kipekecha majani ya juu mweupe

Scirpophaga excerptalis

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Moyo uliokufa.
  • Msururu wa mashimo sambamba kwenye jani.
  • Ulaji ndani ya shina, sehemu zinazo kua na majani.
  • Nondo mwenye rangi ya fedha nyeupe.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Muwa

Dalili

Msururu wa mashimo sambamba kwenye ubapa wa jani wakati linapofunuka ni dalili dhahiri ya shughuli ya vipekecha majani wa juu. Mishipa ya katikati ya majani ina vihandaki vya kahawia vilivyokauka ambayo ndiyo dalili bainifu zaidi ya kutambua hatua ya awali ya mashambulizi. Makundi ya mayai yapo kwenye upande wa juu wa jani karibu na sehemu ya ukuaji. Sehemu zinazokua zinashambuliwa, na kuua shina. Miwa huwa na moyo uliokufa na huwa na rangi nyekundu ya kahawia. Chipukizi la juu hunyauka na kudumaa. Kutokana na ukuaji wa machipukizi ya pembeni mmea huonekana wenye vitita vya majani. Mashimo madogo yanaweza kuonekana kwenye shina karibu na usawa wa ardhi. Ni lava mmoja tu anayekula ndani kwa shina moja.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Kutolewa kwa vidusiai vya mayai kama Trichogramma chilonis @ 10,000/ha mara 2-3 kwa muda wa siku 10 au Ichneumonid parasitised Gambroides (isotima) Javensis (100pairs/ha) wanaweza kuanzishwa kama vidusia wa kudumu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Sambaza viua wadudu kama vile carbofuran 5% G (33.3 kg/ha), au nyunyiza chlorantraniliprole 18.5% SC (375 ml/ha). Matumizi yanaweza kufanywa kwa kufungua mfereji mdogo karibu na eneo la mizizi, kuweka chengachenga za carbofuran, zikifuatiwa na umwagiliaji wa mwanga. Ingawa, ukataji kwa mikono wa mashina machanga yaliyo athiriwa ni mzuri zaidi.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu unafanywa na Kipekecha Majani ya Juu Mweupe wa Miwa, Scirpophaga excerptalis. Nondo aliyekomaa ana mbawa nyeupe za fedha na ncha zenye manyoya. Jike hutaga mayai ambayo yamefunikwa na nywele za manjano-kahawia au uvimbe. Handaki la lava kupitia majani yaliyo virigwa, na kusababisha uharibifu ulioelezwa. Lava wana urefu wa milimita 35 hivi, na vichwa vya rangi ya maziwa au njano na kahawia, visivyo na michirizi, na miguu iliyo dhoofika. Wanakula zaidi kando ya mshipa mkuu wa katikati wa jani na keelekea ndani ya moyo wa mmea. Kizazi cha tatu husababisha hasara kubwa zaidi katika miwa. Mimea michanga huathirika zaidi na wadudu hasa katika mazingira yenye unyevunyevu.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina zinazostahimili au sugu kama CO 419, CO 745, CO 6516, CO 859, CO 1158 au CO 7224 ikiwa zinapatikana.
  • Mifumo ya safu(mistari) zilizounganishwa hupendekezwa katika upandaji.
  • Panda mseto na mimea isiyo shambuliwa kama vile viungo au kunde.
  • Usitumie mahindi, mtama kama mazao mseto.
  • Weka mitego 2-3 ya harufu kwa hekta moja kwenye shamba lako ili kufuatilia nondo waliokomaa.
  • Weka mitego ya mwanga au harufu yenye chaguo lisilonasa maadui wa asili 2 kwa hekta 5.
  • Vinginevyo weka neti za juu asubuhi au wakati wa machweo.
  • Ondoa sehemu za mmea zilizoathirika.
  • Kusanya makundi ya mayai wakati wa utagaji.
  • Pia, haribu mioyo iliyokufa wakati wa kipindi cha pili cha kizazi.
  • Hifadhi wadudu wa asili wanaokula wenzao na vidusia.

Pakua Plantix