Tufaha

Gamba la San Jose

Comstockaspis perniciosa

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Doa lenye mbonyeo mdogo na rangi nyekundu hadi zambarau karibu na maeneo ya kulisha.
  • Utengenezaji wa matunda madogo, yenye umbo lisilo la kawaida na ya rangi iliyofifia.

Inaweza pia kupatikana kwenye

4 Mazao
Tufaha
Aprikoti
Mpichi
Pea

Tufaha

Dalili

Mdudu-gamba hufyonza utomvu kutoka kwenye matawi, majani na matunda. Tabia hii ya ulaji husababisha unyogovu (yaani depression) kidogo na duara la mwanga la rangi nyekundu hadi zambarau kwenye uso wa matunda. Ingawa gamba moja moja haliwezi kuleta uharibifu mkubwa, jike mmoja na kinda lake wanaweza kutoa maelfu kadhaa ya magamba katika msimu mmoja. Wadudu hawa hasa huishi katika miti mikubwa mikongwe ambayo ni vigumu kupata upuliziaji mzuri wa dawa, lakini miti michanga iliyopuliziwa dawa inaweza pia kuathirika. Ingawaje kimsingi wanaishi kwenye magome ya miti, chini ya magamba na kwenye nyufa, dalili ya kwanza kwenye shamba la miti inaweza kuwa madoa madogo mekundu kwenye matunda na majani. Uharibifu wa matunda kwa kawaida hukusanyika pamoja chini ya tunda lililoathirika. Ikiwa shambulio linatokea mwanzoni mwa msimu, matunda yanaweza kuwa madogo au kuwa na umbo lisilo la kawaida. Hali hii hatimae husababisha kupungua kwa jumla kwa uimara ya mmea, ukuaji, na mavuno.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Anzisha maadui wa asili ambao hula wadudu-gamba San Jose. Maadui hawa wa asili ni kama vile mbawakawa/kombamwiko jike mwenye madoa mawili au Cybocephalus californicus. Zaidi ya hayo, chalcids ndogo ndogo na nyigu aphelinid huharibu mizani. Nyunyizia 2% mafuta ya bustani kabla au mara tu baada ya mapumziko ya buds, lakini kabla ya maua kuanza kuchipua. Aphytis Spp., Encarsia Perniciosi na Coccinella Infernalis Mulsant kama wanyama wanaokula wenzao wanatambulika kama mawakala wa kudhibiti kibiolojia wanaofaidi. Chapisha vimelea kama vile Encarsia Pernicious 2000 kwa miti iliyoshambuliwa mara moja wakati wa majira ya kuchipua katika maeneo yaliyoathirika.

Udhibiti wa Kemikali

Wakati wote zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia, ikiwa yanapatikana. Dhibiti idadi kubwa ya wadudu kwa kutumia dawa ya kuua wadudu pamoja na kupulizia mafuta katika kipindi kilichochelewesha ukuaji wa wadudu. Tumia Viua wadudu vyenye vidhibiti vya ukuaji wa wadudu kama vile pyriproxyfen au buprofezin, neonicotinoids, organofosfati au spirotetramat pale unapoona wadudu waliopevuka kwenye mitego ya pheromone au watambaazi wa kwanza kwenye kanda za kunata. Endelea na unyuniziaji katika siku 10 baadaye ikiwa utaendelea kupata watambaaji amilifu.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na mdudu mharibifu wa miti ya matunda anayefahamika kama Gamba la San Jose. Wadudu majike ni wa manjano, hawana mabawa na ni laini, wenye umbo la tufe. Wadudu hawa wana urefu wa takribani milimeta 1.5 hadi 2.2 na utepe mweusi upande wa nyuma. Wadudu wachanga hupitia hatua tatu za mtambaazi(mdudu anayetambaa), nta mweupe unaofahamika kama kofia nyeupe na nta mweusi, yaani kofia nyeusi. Mdudu mchanga anaweza kukamilisha mzunguko wake wa maisha katika takriban siku 37, na vizazi viwili vya wadudu kila mwaka. Ukuaji wa wadudu huanza tena majira ya kuchipua wakati halijoto inapozidi 11°C. Wadudu wachanga wanaoishi msimu wote wa baridi wanakuwa amilifu katikati ya mwezi wa Machi na madume huibuka mwezi wa Aprili. Majike ni ovo-viviparous, yaani huzaa kwa kutaga na kuangua mayai ndani kwa ndani, na huzaliana katikati ya Mei na kuzalisha vichanga 200 na 400 kwa mwezi. Mzunguko wa kawaida wa maisha hukamilika kwa siku 35-40, na wadudu huanza kukua wakati wa majira ya maua. Mdudu-gamba wa kike ni wa duara, iliyobinuka kidogo ikiwa na malengelenge meusi wakati dume ni wa mstari.


Hatua za Kuzuia

  • Usafi wa shamba la matunda unapaswa kupewa kipaumbele cha juu.
  • Uondoaji wa kawaida wa mimea mbadala inayoweza kubeba wadudu, uondoaji wa magugu, mimea inayoota yenyewe, pamoja na mabaki ya mazao, ni hatua inayoweza kupunguza sana uwezekano wa mashambulizi ya wadudu wa magonjwa.
  • Matawi yaliyoshambuliwa sana yanapaswa kukatwa, kuchomwa moto na kuharibiwa.
  • Chunguza miti kwa uangalifu wakati inaposinzia kukua ili kujua kiwango cha mashambulizi.
  • Fuatilia kwa umakini miti inayohifadhi majani wakati wa majira ya baridi kwani hii ni dalili nzuri ya kuwepo kwa wadudu.
  • Tumia mitego ya kemikali za pheromone kugundua uwepo wa mimea dume.
  • Weka mitego upande wa kaskazini na mashariki wa miti kwa urefu wa futi sita hadi saba, na uangalie kila wiki.
  • Matawi yaliyoshambuliwa yanapaswa kukatwa ili kupunguza idadi ya wadudu wa magonjwa na kuboresha kupenya kwa upuliziaji.
  • Pulizia mafuta ya kudhibiti wadudu wakati vichipukizi vinaonyesha ukijani lakini kabla ya kugeuka na kuwa rangi ya waridi.
  • Uwekaji wa dawa za kuua wadudu unaweza kudhibiti wadudu wapya wanaotambaa wanaoibuka mwanzoni mwa kiangazi.

Pakua Plantix