Bagrada hilaris
Mdudu
Majani, shina, na maua huonyesha uharibifu unaotokana na kuliwa. Kuliwa kwa majani yaliyokomaa husababisha makovu meupe kwenye pande zote za majani. Majani membamba yanaweza kuanza kuwa na mabaka meupe kama karatasi. Mimea iliyoathirika inaonyesha dalili za kunyauka, kubadilika rangi na kuwa ya njano, na kukauka kwa majani. Sehemu za ukuaji wa mmea (kwnye ncha ya tawi) zinaweza kufa, na mimea michanga inaweza kushindwa kuhimili mashambulizi ya wadudu na hivyo kusababisha kifo cha mimea. Uharibifu pia unaweza kuathiri mazao yaliyo vunwa. Mazao haya yanaweza kuwa madogo kwa umbo, kuwa na vichwa vya kabichi visivyoweza kuuzika au kutokuwa na vichwa kabisa (vinavyojulikana kama mimea "kipofu"). Wadudu waliopevuka na tunutu (wadudu wachanga) wote hufyonza majimaji/utomvu kutoka kwenye sehemu zote za mmea. Wadudu waliokomaa pia hutoa dutu inayoganda ambayo huharibu mazao.
Wadudu kadhaa kutoka familia ya nyingu vidusia wanaweza kushambulia mayai ya Bagrada hilaris, na wadudu hawa ni kama vile Gryon, Ooencyrtus, Telenomus, na Trissolcus. Wadudu waliokomaa hushambuliwa na nzi na buibui. Upuliziaji wa mchanganyiko wa sabuni umeonekana kuwa na ufanisi dhidi ya wadudu hawa. Changanya pilipili, sabuni, vitunguu swaumu, na mafuta ya taa kisha mchanganyiko wake pulizia kwenye mazao yako.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Panda mbegu zilizotibiwa na imidacloprid. Tumia dawa za kuua wadudu zinazogusa majani kwenye miche michanga wakati wa mchana na jioni mapema. Madawa ya Pyrethroids, pyrethrins, neonicotinoids, na organophosphate yamekuwa na ufanisi dhidi ya wadudu hawa.
Uharibifu husababishwa na wadudu waliokomaa na tunutu (wadudu vijana) waitwao Bagrada hilaris, anayejulikana pia kama Bagrada au Mdudu/mende wa Rangi. Mdudu aliyepevuka ni mweusi na pia ana alama za rangi nyeupe na machungwa kwenye mwili wake, ambao umeundwa kama ngao. Kipimo cha mdudu huyu ni takribani milimita 5-7. Wadudu hutaga mayai yao kwa makundi kwenye majani au kwenye udongo karibu na mimea. Mwanzoni, wadudu wachanga huwa hawana mbawa na wanakuwa na rangi ya machungwa inayong'aa. Kadri wanavyokua, wanabadilika na kuwa wekundu na kupata alama zenye rangi ya weusi hadi wanavyoonekana kama umbo la wadudu kamili. Wadudu hawa huathiri zaidi mimea hasa kutoka familia ya Mharadali (Brassica), kama vile kabichi, koliflawa, na kale. Mimea hii mara nyingi huathirika kutokana na joto na ukosefu wa maji. Wadudu hawa huidhuru mimea kwa kufyonza maji maji kutoka kwenye majani na kuishambulia kwa idadi kubwa.