Megachile sp.
Mdudu
Dalili zinajitokeza tu kwenye majani. Mashimo ya duara hadi mviringo yanaweza kuonekana kwenye kingo za majani.
Hakuna matibabu yanayohitajika.
Kwa kuwa nyuki hawa ni wachavushaji bora kwa mazao yako, haishauriwi kutumia mbinu kali au hatua kali za kudhibiti.
Dalili hizi husababishwa na nyuki wanaoishi pweke (sio kwa makundi) wanaotoka kwenye familia ya Megachile. Nyuki hawa hukata majani kuwa vipande na kuyapeleka kwenye viota vyao. Nyuki jike kamili (aliyepevuka) hujenga viota kwa kutumia majani yaliyo katwa; majani ambayo hugawanywa katika seli(vichumba vidogo) na hutaga yai moja katika kila seli/kichumba. Baada ya kujivua ngozi mara chache, lava hutengeneza ganda na kuingia kwenye hatua ya pupa. Hutokea kutoka kwenye kifaranga kama mzazi. Dume hufa muda mfupi baada ya kujamiiana, lakini jike huishi kwa wiki chache zaidi, kipindi ambacho huunda viota vipya. Hawasababishi uharibifu wa kiuchumi.