Procontarinia
Mdudu
Dalili huonekana zaidi kwenye majani, lakini pia mara chache kwenye vichipukizi, maua, na matunda machanga ya miti ya maembe. Sehemu zilizoathiriwa na nzi wa usubi hufunikwa na vijipu vidogo vingi vilivyochomoza au uvimbe. Kila kijipu kinachofanana na chunusi au uvimbe ni cha ukubwa wa mm 3-4 na ndani yake kuna lava wa rangi ya njano anayekula tishu za mti. Katika hatua za awali, sehemu ya kutagia mayai huonekana kama doa jekundu dogo. Majani yaliyoathirika sana yanaweza kupinda, kupunguza kiwango cha usanisinuru, na kuanguka mapema. Maua yaliyoathirika yanaweza kushindwa kufunguka. Mashimo madogo ya kutokea upande wa chini wa majani ni mabaki yanayosababishwa na kuwepo kwa lava. Mashimo haya ya kutokea yanaweza kusababisha maambukizi ya kuvu wa upili. Matunda machanga pia huonyesha mashimo ya kutokea kwenye sehemu ya shina. Machipukizi ya maembe yaliyoathiriwa sana huwa na maua machache sana, jambo ambalo linaweza kupunguza mavuno kwa kiasi kikubwa.
Wadudu wa utando wa kuanguka, Tetrastichus sp., wanawinda lava wa Procontarinia sp. na hivyo wanaweza kutumika kudhibiti wadudu hawa. Wengine ni vidusia wa familia ya Platygaster sp., Aprostocetus spp., na Systasis dasyneurae. Tumia kiziduo cha mbegu za mwarobaini juu ya mwavuli wa mti.
Kila wakati zingatia mbinu jumuishi kwa kuchukua hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaolojia, ikiwa yanapatikana. Matumizi yaliyo zidi ya dawa za kuua wadudu yanaweza kusababisha ukinzani na kuua maadui wa asili. Kunyunyizia 0.05% fenitrothion wakati wa kuota kwa vichipukizi kunaweza kuwa na ufanisi katika kudhibiti wadudu. Matumizi ya bifenthrin kwenye majani (70ml/100l) iliyochanganywa na maji pia yameonyesha matokeo mazuri. Unyunyiziaji wa dawa hii unapaswa kurudiwa kila baada ya siku 7-10 katika msimu wa maua hadi matunda yanapofikia ukubwa wa njegere.
Dalili husababishwa na aina tofauti za nzi wa usubi, Procontarinia sp. Nzi kamili ni wa ukubwa wa mm 1-2 na hufa ndani ya masaa 24 baada ya kuangua, kujamiiana na kutaga mayai. Mayai hutagwa kwenye sehemu mbalimbali za mti, lakini hasa hupatikana kwenye majani. Wakati yanapo angua, lava wanaingia kwenye tishu na kuleta uharibifu kulingana na sehemu wanayoathiri. Sehemu za maua zinazokaliwa zinaweza kukauka na kuanguka chini kutokana na ulaji mkubwa. Lava waliokomaa huhamia au kuanguka kwenye tabaka la juu la udongo, ambapo wanaingia kwenye hatua ya pupa. Kuibuka kwa nzi kamili kwa kawaida hufanyika mchana na hupelekewa na hali ya baridi (20°C) na unyevunyevu wa 60-82%. Kunaweza kuwa na vizazi 3-4 vya wadudu katika kipindi cha Januari hadi Machi kwenye kizio cha kaskazini.