Embe

Nondo wa Kiwavi Konokono

Limacodidae sp.

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Majani yaliyotafunwa.
  • Kuwepo kwa viwavi.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Embe

Dalili

Viwavi konokono husababisha kupotea kwa majani kwa kuyala. Viwavi hao hula kiasi kikubwa cha tishu za mimea na kuacha mishipa na mashina tu. Kutokana na hilo, mimea inakuwa haina uwezo wa kufanya usanidi wa mwanga (photosynthesis) kwa usahihi, na hivyo kusababisha mavuno kidogo kwenye mazao. Hii inamaanisha kwamba mimea iliyoathirika inaweza kutoa matunda machache kuliko ambavyo yangepatikana endapo ingekuwa haijaathiriwa viwavi.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Ili kudhibiti wadudu bila kutumia kemikali, inashauriwa kuondoa viwavi kwa njia ya kawaida kutoka kwenye mimea iliyoathirika. Kazi hii ya kuondoa viwavi inapaswa kufanywa kwa kutumia koleo au kipande cha utepe(tepu) bila kuwigusa moja kwa moja. Mitego ya mwanga pia inaweza kutegwa ili kuwadaka na kuwakusanya nondo kamili. Takriban mitego 5 ya mwanga inaweza kutegwa kwa kila hekta moja ili kudhibiti wadudu kwa ufanisi. Hii ni njia nzuri ya kupunguza idadi ya viwavi bila kuathiri mazingira.

Udhibiti wa Kemikali

Chagua dawa ya kuua wadudu inayofaa kwa mahitaji yako maalumu, kwa kufuata kwa uangalifu maagizo ya lebo, na kuvaa mavazi ya kujikinga pamoja na glavu wakati wa kuitumia. Viambato hai viwili ambavyo ni Carbaryl na Dichlorvos vimeripotiwa kuwa na ufanisi mzuri katika kudhibiti viwavi hawa.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu unaosababishwa na viwavi konokono unatokana na viwavi wa nondo wa familia ya Limacodidae. Viwavi hawa wanajulikana kwa mwonekano wao unaofanana na konokono, na wanaweza kuwa tatizo la kiafya kwa binadamu kutokana na kuwa na mwiba makali uliopo kwa aina nyingi za familia hii ya viwavi. Aidha, viwavi hawa wapo kwa wingi kwenye maeneo ya tropiki ambako wanapatikana mwaka mzima. Viwavi konokono hupitia hatua kadhaa katika mzunguko wao wa maisha. Mzunguko huanza na mayai ambayo hutagwa kwenye majani ya mimea. Mara mayai yanapoanguliwa, viwavi wadogo huanza kula majani. Wakati wa ukuaji wao, hujibadilishia ngozi mara kadhaa na kubaki na ngozi mpya. Hatimaye, hutengeneza vifukofuko na kujizungushia na kuingia katika hatua ya pupa. Baada ya muda, nondo kamili hutoka kwenye vifukofuko na kuanzisha tena mzunguko huu wa maisha. Wadudu hawa wana umuhimu mkubwa kiikolojia kwa mimea jamii ya michikichi kwa sababu wanaweza kusababisha upukutikaji mkubwa wa majani. Ni muhimu kuwabaini na kuwadhibiti mapema ili kuzuia uharibifu wa mazao na kuhakikisha ukuaji mzuri wa mimea.


Hatua za Kuzuia

  • Ili kuzuia uvamizi wa viwavi konokono, ni muhimu kuhakikisha mimea yako inakuwa na afya na haijaharibiwa.
  • Nunua mbegu kutoka kwa wasambazaji safi na wanaotambuliwa rasmi tu, na inapendelewa zaidi mbegu ambazo zimethibitishwa.
  • Utambuzi wa mapema wa wadudu waharibifu ni muhimu sana.
  • Chunguza mashimo yaliyotafunwa kwenye majani, ambayo yanaweza kuashiria uwepo wa viwavi.
  • Ili kuwa na uhakika kwamba Viwavi Konokono wa Nondo wanatokea kweli, nondo na viwavi wanapaswa pia kugunduliwa kwenye shamba.
  • Uharibifu wa majani na kupukutika kwa majani pia kunaweza kusababishwa na wadudu wengine waharibu.

Pakua Plantix