Embe

Maji Moto

Oecophylla smaragdina

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Majani yaliyofunikwa kwa utando na vitu vyeupe.
  • Maji moto/chungu wenye rangi ya machungwa.
  • Viota vinapatikana kwenye miti ya msituni, lakini vinaweza pia kupatikana kwenye nyufa za juu kama vile paa na nguzo za simu na umeme.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Embe

Dalili

Majani yanafumwa pamoja na vitu vyeupe mithili ya karatasi, yakitengeneza kiota cha maji moto. Kiota kinaweza kuwa kikubwa kama ngumi au kichwa cha binadamu. Vidukari na vidugamba wanaweza kuwapo karibu na viota. Maji moto wanajulikana zaidi kwa ujenzi wao wa kipekee wa viota. Maji moto hawa huunda minyororo imara ya maji moto kwa kuunganisha miguu yao ili kuvuta na kuyapinda majani kwenye mwelekeo wautakao wa mithili ya hema, kwa kutumia uratibu wa hali ya juu. Kisha maji moto hutumia lava wao wenyewe kutoa hariri ambayo hutumika kushona majani pamoja ili kuunda kiota. Viota kadhaa vinaweza kuwepo kwenye mti kwa wakati mmoja.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Wanyama wa asili kama Agama agama, Geocoris ochropterus, Niphopyrallis chionesis na vimelea kama Smicromorpha keralensis husaidia kudhibiti idadi ya wadudu. Bacillus thuringiensis umekuwa na mafanikio katika kupunguza matukio ya wadudu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Upuliziaji wa dawa za kikemikali unapaswa kuzingatia kuondoa viota kwani siafu watengenezaji wa matundu ni wakala wa kibayolojia.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na maji moto/chungu wanaofahamika kitaalaamu kama, Oecophylla smaragdina. Jina lao linatokana na rangi ya kijani ya malkia wao.maji moto hawa mara nyingi hutumika kama mawakala wa udhibiti wa kibaiolojia dhidi ya wadudu wengine waharibifu, wakila wadudu wadogo au arthropodi. Kwa kuwa wanaishi katika uhusiano wa pande mbili na vidukari na vidugamba ili kula asali ya mimea, inaweza kusababisha uharibifu usio wa moja kwa moja. Makoloni/idadi yao inaweza kuwa na ukubwa wa takribani nusu milioni ya maji moto, maji moto wafanyakazi wana ukubwa wa ama milimita 5-6 au milimita 8-10, na wana rangi ya machungwa. Viota hujengwa wakati wa usiku kwa msaada wa lava wazalisha hariri. Maji moto wanapatikana zaidi katika ukanda wenye hali ya hewa ya kitropiki ya Asia, Australia, na Pasifiki ya Magharibi. Mwiba wa maji moto ni wa maumivu. Kwa kawaida maji moto huwa na urefu wa takribani milimita 20-25. Kwa kawaida wana rangi mithili ya kijani kawahia. Maji moto ni washari kwenye himaya zao na wamekuwa wakitumika kudhibiti wadudu waharibifu kwenye kilimo kwa miaka mingi. Majimoto wana mshiko mkali na nguvu kubwa sana.


Hatua za Kuzuia

  • Ondoa kwa uangalifu na haribu viota vya maji moto mara kwa mara.
  • Tengeneza moshi ili kuwafukuza maji moto ikiwa kiota ni kidogo, na kisha ondoa viota.

Pakua Plantix