Aulacophora foveicollis
Mdudu
Wadudu kamili wanakula kwa uroho majani, maua na matunda. Mbawakawa huyu huchimba mashimo makubwa kwenye tishu za mimea (kati ya mishipa ya majani), na hivyo kusababisha ukuaji kudumaa na hatimaye kifo cha mimea. Uharibifu unaofanywa kwenye miche midogo mara nyingi unakuwa mbaya kwani uchelewesha kukomaa kwa mazao. Endapo maua yameathirika, itasababisha kupungua kwa utengenezaji wa matunda. Funza wa mdudu huyu hubaki kwenye udongo na kula mizizi na mashina ya mimea yaliyo chini ya ardhi, jambo linalosababisha kuoza na kunyauka kwa mashina na mizizi. Wadudu kamili wanaokula miche wanaweza kudumaza ukuaji na hata kusababisha kifo, na hivyo kusababisha mabaka matupu shambani. Wakati mwingine mbawakawa hukusanyika na kutafuna majani ya mimea mikubwa. Sehemu za maua pia zinaweza kukumbwa na uharibifu, na hivyo kusababisha kupungua kwa utengenezwaji wa matunda. Sehemu za chini za matunda machanga zinaonyesha makovu yanayosababishwa na ulaji wa wadudu kamili, na kuwezesha uvamizi wa vijidudu vinavyosababisha kuoza.
Wadudu wanaokula mbawakawa, wakiwemo wanachama wa familia ya tachinid na reduviid Rhynocoris fuscipes. Changanya nusu kikombe cha majivu ya kuni na nusu kikombe cha chokaa kwenye lita 4 za maji, na kisha acha mchanganyiko utulie kwa saa chache. Chuja na ujaribu mchanganyiko huu kwenye mimea michache iliyoathiriwa kabla ya kutumia shambani. Tumia mchanganyiko huu kama dawa ya kupulizia majani kwenye mazao yako. Vinginevyo, unaweza kutumia dawa zinazotokana na mimea kama vile mwarobaini (NSKE 5%), derris au pareto(ongeza na sabuni) kila baada ya siku 7. Tumia Tricoderma Trichoderma kwa ajili ya kutibu mbegu na kitalu, na Pseudomonas fluorescens kama tiba ya mbegu, kitalu na kutumia kwenye udongo. Tumia mimea ya mtego iliyotibiwa kwa dawa kali za kuua wadudu ili kuvutia na kuua mbawakawa (mbawakavu).
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia, ikiwa yanapatikana. Dawa ya kuua wadudu aina ya Deltamethrin, kwa kipimo cha mililita 250 kwa eka inaweza kutumika ikiwa inagundulika uwiano uliopo ni mbawakawa mmoja kwa kila mimea 10 kwenye kitalu. Dawa za kuua wadudu zinazotokana na maua ya pareto zina uwezekano wa kufanya kazi kwa ufanisi lakini pia dawa hizi ni hatari kwa wadudu wanaokula wadudu waharibifu(Maadui wa asili). Matumizi ya mimea ya mtego iliyotibiwa kwa dawa kali za kuua wadudu inaweza kuvutia na kuua mbawakawa kamili. Pulizia fenitrothion mara tu wadudu wanapogunduliwa na rudia mchakato huu kila baada ya siku 15.
Uharibifu husababishwa na funza pamoja na mbawakawa kamili wanaofahamika kama Aulacophora foveicollis, ambao hula majani, maua, na matunda. Lava waliokua huwa na rangi ya krimu nyeupe na ukubwa wa ukucha wa binadamu. Mayai kwa kawaida huwa ya mviringo, yenye rangi ya manjano na hutagwa moja moja au kwa makundi ya mayai 10 kwenye udongo wenye unyevunyevu, katika kina kinachoweza kuzama kidole cha binadamu karibu na kitako cha mmea. Mbawakawa kamili wana rangi ya chungwa-nyekundu na ukubwa sawa na nzi wa nyumbani. Viwavi huanguliwa baada ya wiki 1 au 2 na hushambulia mimea na mizizi yake kabla ya kuingia kwenye udongo na kuwa pupa. Hatua ya kubadilika toka kuwa pupa hadi mbawakawa hufanyika katika kifuko kwenye udongo kwa muda wa siku 7 hadi 17. Hali bora ya mazingira ya kuwezesha kubadilika kuwa mbawakawa hupatikana wakati joto linapokuwa nyuzi 27-28°C.