Helicoverpa armigera
Mdudu
Mayai yenye rangi nyeupe hadi kahawia yanaweza kupatikana kwa vikundi kuzunguka maeneo ya maua na majani mapya kwenye sehemu ya juu ya shada la majani. Uharibifu wa ulaji unaweza kuonekana kwenye tishu zozote za mmea, lakini zaidi kwenye maua na vitumba/masuke/matunda/maganda, kutegemea na mmea unaohifadhi vimelea. Viwavi wadogo hukwangua majani, sehemu za ukuaji, au sehemu inayotoa matunda, na hivyo kusababisha uharibifu mdogo. Viwavi wakubwa hutoboa maua au vitumba vichanga/mashuke/matunda/maganda, na kutengeneza shimo kutokea ndani, kuharibu mbegu na kuzifanya zifae kwa kuuza. Vinyesi vya wadudu huonekana karibu na mashimo yanayotokana na kula. Ukuaji wa vimelea vya pili kwenye majeraha husababisha kuoza kwa tishu zilizoathirika.
Nyigu jamii ya Trichogramma (T. chilonis au T. brasiliensis) wanaweza kutumika wakati wa mwanzo wa kutoka maua ili kushambulia mayai. Aidha, manyigu jamii ya ya Microplitis, Heteropelma, na Netelia hushambulia lava. Wadudu wanaokula wadudu wengine (kama vile mdudu mwenye macho makubwa, yaani big-eyed bug, mdudu askari wa kahawia, yaani glossy shield bug, na mdudu askari mwenye mdomo wa miiba), wadudu jamii ya mchwa, buibui, mdudu koleo, chenene, na wadudu jamii ya nzi hushambulia lava na hivyo wanapaswa kuzingatiwa kutumika kwa udhibiti wa kibaiolojia. Tumia dawa za kuua wadudu za kibaolojia zinazotokana na spinosad(kemikali za kwenye bakteria), nucleopolyhedrovirus (NPV), Metarhizium anisopliae, Beauveria bassiana, au Bacillus thuringiensis ili kudhibiti lava. Dawa zinazotokana na mime kama vile mafuta ya mwarobaini, kiziduo (ukamuaji) cha mbegu za Mwarobaini (NSKE 5%), pilipili, au vitunguu swaumu, vinaweza kutumika kama dawa ya kupulizia majani wakati wa hatua ya utokaji wa jicho la ua.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na tiba za kibaolojia ikiwa zinapatikana. Dawa za kuua wadudu kwa kuchagua (maalumu kwa wadudu jamii ya funza wa vitumba) ndiyo chaguo bora la kuondoa wadudu shambani bila kuathiri wadudu wenye manufaa. Ufuatiliaji ili kubaini mayai na lava ni muhimu kwa sababu viwavi huwa wanakuwa na uwezo wa kuhimili dawa za wadudu. Dawa zinazotokana na chlorantraniliprole, chloropyrifos, cypermethrin, alpha- na zeta-cypermethrin, emamectin benzoate, esfenvalerate, flubendiamide, au indoxacarb zinaweza kutumika (kwa kawaida @ 2.5 ml/l). Matumizi ya kwanza yanapaswa kuwa katika hatua ya kutoka maua na kufuatiwa na kupuliza kila baada ya siku 10-15. Matibabu ya kemikali huenda yasiwe na tija kwa mazao yenye thamani ndogo.
Uharibifu unasababishwa na funza wa vitumba (kitaalamu Helicoverpa armigera) , ambaye ni mdudu wa kawaida kwa aina mbalimbali za mazao. Funza huyu ni mojawapo ya wadudu waharibifu zaidi katika kilimo. Nondo wanakuwa na rangi ya kahawia iliyofifia na urefu wa sentimita 3-4 kutoka mwisho wa bawa moja hado lingine. Kwa kawaida wana mbawa za mbele zenye rangi ya manjano hadi machungwa au kahawia, yakiwa na nakshi ya madoa yenye rangi ya giza. Mbawa za nyuma ni nyeupe, zikiwa na mishipa (vena) yenye rangi ya giza na madoa marefu yenye rangi ya giza kwenye kingo za chini. Majike hutaga mayai meupe ya mviringo,na hutaga kika mmoha peke yake au kwa makundi kwenye maua au ubapa wa majani, hususani kwenye kanopi ya juu. Lava wana rangi ya kijani mzeituni hadi kahawia iliyokolea, kutegemea na hatua ya upevukaji. Miili yao ina madoa madogo ya rangi ya nyeusi na wana kichwa chenye rangi ya giza. Katika hatua za baadaye za upevukaji/ukomavu, mistari na mikanda huonekana mgongoni na ubavuni mwao. Wanapofikia ukomavu, hujificha kwenye udongo kama pupa. Kwa kawaida idadi ya wadudu huwa ya juu zaidi wakati wa ukuaji wa matunda, maganda, na vitumba, jambo ambalo husababisha upotevu mkubwa wa mavuno.