Myllocerus sp.
Mdudu
Dalili za kwanza za mashambulizi ya fukusi wa kijivu ni kuonekana kwa kingo za majani zilizokatika kwa umbo la V. Fukusi wakubwa hupendelea kula kwenye kingo za mimea michanga na kisha kuendelea ndani. Majani yaliyoathiriwa sana yote yanaweza kupukutika. Mimea yenye afya itaweza kupona kutokana na uharibifu wa kuliwa, lakini miche michanga itakufa wakati wa kuchanua maua. Mashambulizi makubwa yanaweza kuzuia ukuaji wa mmea. Mimea iliyoathiriwa inaweza kung’olewa kwa urahisi.
Pulizia udongo wako kwa Bacillus thuringiensis, spishi ndogo ya tenebrionis (Btt) kwa kipimo cha 2.5 mg/lita. Bakteria pia wanaweza kutumika kwa njia ya kuchovya mizizi. Unachovya mizizi ya mmea wako kwenye mchanganyiko wa Btt na kuikausha kwa njia ya hewa kabla ya kuipanda tena kwenye udongo. Kiwango cha vifo vya funza kinategemea na utunzaji wa unyevu na joto. Tumia keki ya mwarobaini kwa kipimo cha kilo 500/hekta wakati wa kulima kwa mara ya mwisho.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye kutumia hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia, ikiwa yanapatikana. Matibabu ya kemikali yana mafanikio kidogo tu katika kudhibiti fukusi wa kijivu kwa sababu mayai, lava, na buu wao wanakuwa kwenye udongo.Fukusi wakubwa vilevile ni vigumu kuwadhibiti kutokana na uwezo wao wa kuruka, kujificha, na kujifanya wamekufa. Matatizo hujitokeza na ukuaji wa usugu. Unaweza kupulizia dawa aina ya quinalphos au chlorpyrifos siku 20 baada ya kupanda.
Dalili husababishwa na fukusi wakubwa na funza wa fukusi wa kijivu. Fukusi wakubwa ni wadogo kwa umbo na wana rangi ya kijivu iliyofifia, na michoro ya giza kwenye mbawa na vichwa vyao. Majike hutaga wastani wa mayai 360 kwenye udongo kwa kipindi cha siku 24. Baada ya kuanguliwa, lava huchimba kwenye udongo ambako hula mizizi ya mimea. Hatimae funza huzaliana kwenye udongo. Fukusi wakubwa watabaki hai wakati wa majira ya baridi, wakijificha chini ya mabaki. Fukusi wa Pua Pana wana wigo mpana wa mimea wanamoweza kuishi, kuanzia mimea ya mapambo, mboga hadi spishi za matunda.