Tikiti

Kiwavi wa Maboga

Diaphania indica

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Majani yaliyojivingirisha na nyuzi za hariri.
  • Mashimo kwenye matunda yanayoendelea kukua.

Inaweza pia kupatikana kwenye

7 Mazao

Tikiti

Dalili

Lava mchanga hukwangua sehemu ya klorofili kutoka kwenye majani. Baadaye, anayakunja majani hayo na kuyazungushia utando. Viwavi hushambulia pia maua na matunda yanayoendelea kukua. Wanaharibu ngozi ya matunda, na kusababisha matunda hayo kuoza. Kutokana na kukwanguliwa, majani hukauka katika hatua za baadaye. Katika hali ya mashambulio makubwa, mashimo yanaweza kuonekana kwenye matunda yanayokua.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Tumia dawa za kuua wadudu za kibaiolojia kama vile Bacillus thuringiensis na Beauveria bassiana. Tumia bidhaa za madawa yanayotokana na mimea kama vile mwarobaini, Derris (mkundekunde), Pareto, na pilipili. Chochea shughuli za wadudu vimelea kama vile Apanteles spp. Nyunyiza mchanganyiko uliozimuliwa wa maji na mkojo wa ng'ombe ili kufukuza wadudu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiolojia, ikiwa yanapatikana. Nyunyiza dawa za kuua wadudu katika hatua za awali za utengenezwaji wa matunda ili kuepuka hasara ya mavuno. Tumia dawa za kuua wadudu zilizopendekezwa kwenye majani na matunda machanga.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na lava mchanga wa kiwavi. Nondo kamili ana mabawa meupe yanayopitisha mwanga na madoa meusi mapana kwenye kingo, na nondo majike wana kishungi chenye nywele za rangi ya chungwa kwenye sehemu ya mwisho ya mkundu. Mayai hutagwa moja moja au kwa makundi kwenye upande wa chini wa majani kwa siku 3-4. Kwa kawaida kiwavi huonekana amerefuka huku akiwa na jozi ya michirizi iliyo wima sambamba na mstari wa kati wa nyuma. Kiwavi hufikia hatua ya kuwa mdudu/nondo kamili (aliyepevuka) katika takriban siku 10.


Hatua za Kuzuia

  • Fuatilia majani machanga ili kuona uwepo wa vishipajani, lakini sehemu za katikati zikiwa zimeliwa.
  • Tafuta vinyesi kwenye majani.
  • Kusanya na angamiza viwavi vilivyo kwenye hatua za awali za ukuaji.
  • Ondoa majani yaliyojivingirisha na waue viwavi walioko ndani kwa kuwaminya.

Pakua Plantix