Pamba

Fukuzi (Fukusi) wa Shina la Pamba

Pempherulus affinis

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Uvimbaji mithili ya fundo kwenye shina, juu kidogo ya ardhi.
  • Kunyauka na kukauka kwa mmea.
  • Ukuaji uliodumaa.
  • Mashina yanaweza kuanguka kwa urahisi.
  • Mimea michanga inakufa.
  • Vidogo, vya vyeusi na vina namna ya rangi nyeupe kwenye mabawa yao na kichwa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Pamba

Dalili

Dalili inayotambulika zaidi ya uvamizi wa dumuzi wa shina la pamba ni uvimbaji wa shina unaokuwa mithili ya fundo, juu kidogo ya ardhi. Hii inatokana na uharibifu wa tishu za mishipa unaosababishwa na lava wanaokula ndani ya shina. Mimea michanga hufa kila mara kutokana na athari za uharibifu huo. Mimea ya iliyokomaa huonyesha dalili za kunyauka kwanza na kisha kukauka polepole. Ina uwezekano mkubwa wa kuishi lakini itakuwa na uimara mdogo na ukuaji wa kudumaa. Mashina yaliyoathiriwa yanaweza kuanguka kwa urahisi wakati upepo mkali unapovuma au kutokana na uzito wa vitumba vya pamba. Dalili nyingine ni kupungua kwa idadi ya vitumba na ubora duni wa nyuzi za pamba.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Matumizi ya keki ya Mwarobaini kwenye udongo iliyochanganywa na mbolea ya samadi (FYM) wakati wa kuweka mbolea kwenye kitako cha shina inaweza kupunguza uwezekano wa uvamizi wa fukusi wa shina na chipukizi (tani 10 za samadi + kilo 250 za keki ya Mwarobaini/ha). Zaidi ya hayo, mimea michanga inaweza kumwagiwa mchanganyiko wa mafuta ya Mwarobaini ili kuzuia fukusi waliokomaa kutaga mayai kwenye majani. Mitego ya harufu (kemikali inayovutia wadudu waharibifu) inaweza kutumika kwa kufuatilia na kudhibiti fukusi (ikiwa imechanganywa na dawa ya kibaiolojia ya kuua).

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu ya kinga ya mbegu (10 ml ya chlorpyrifos 20 EC/kg ya mbegu) yanaweza kutumika kupunguza kuenea kwa mdudu. Matibabu ya kupulizia sehemu ya shina karibu na ardhi kwa kutumia chlorpyrifos 20 EC pia ni matibabu yenye ufanisi dhidi ya fukusi wa shina na chipukizi (kwa uwiano wa 2.5 ml/L). Mwagilia mimea kila baada ya siku 15, kuanzia siku 15-20 baada ya kuota. Mitego ya harufu(kemikali inayovutia wadudu waharibifu) inaweza kutumika kwa ajili ya kufuatilia na kudhibiti fukusi wa shina (ikiwa imechanganywa na dawa ya kuua wadudu)

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na dumuzi wa shina la pamba ambae kwa kitaalamu anaitwa Pempherulus affinis. Fukusi/Dumuzi waliokomaa ni wadogo, wana rangi ya kahawia iliyokolea, na weupe ang'avu kwenye vifuniko vya mbawa zao na kichwa. Majike hutaga mayai yao kwenye machipukizi yanayokua ya mimea michanga. Baada ya mayai kuanguliwa, funza weupe huchimba kwenye shina kati ya gome na shina, na kuanza kula kwenye tishu za mishipa. Hii husababisha uvimbaji wa kawaida kwenye shina, juu kidogo ya usawa wa ardhi. Fukusi wa chipukizi la pamba (Alcidodes affaber) huonyesha tabia sawa na fukusi wa shina la pamba. Kwa hiyo, hatua sawa za matibabu na kinga zinaweza kutumika dhidi ya fukusi wa shina na yule wa chipukizi la pamba. Hata hivyo, fukusi wa chipukizi la pamba ni wa rangi ya kijivu-kahawia na wenye mkanda wenye rangi hafifu kwenye mbawa zao za mbele. Fukusi wa shina la pamba wakati mwingine wanaweza kuwa mdudu hatari katika baadhi ya maeneo ya Kusini mwa India, hususani Tamil Nadu.


Hatua za Kuzuia

  • Panda kwa kuacha nafasi ndogo kati ya mmea na mmea ili kuzuia mdudu.
  • Pandisha udongo kuzunguka miche kwenye mistrari ili kuzuia fukusi.
  • Punguza wingi wa mazao, kwa mfano kwa kupanga upumzishaji wa shamba au kutumia mzunguko wa mazao.
  • Ondoa mimea mbadala inayohifadhi fukusi ambayo ipo shambani na karibu na shamba (rosella, Indian mallow).
  • Fuatilia mashamba na ondoa mimea iliyoathirika.
  • Ondoa na choma mabaki ya mimea baada ya mavuno.
  • Tumia mitego ya harufu kufuatilia uwepo wa fukusi.

Pakua Plantix