Mti wa jamii ya mchungwa

Mdudu Gamba Mwekundu

Aonidiella aurantii

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Mdudu Gamba Mwekundu hushambulia sehemu zote za juu za mti ikiwemo vitawi vidogo, majani, matawi, na matunda, na hufanya hivyo kwa kufyonya tishu za mmea.
  • Mashambulizi makubwa husababisha majani kuwa ya manjano na kudondoka, kufa kwa vitawi vidogo na matawi makubwa, na wakati mwingine husababisha kifo cha mti.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mti wa jamii ya mchungwa

Dalili

Wadudu gamba wengi wadogo, wenye rangi ya kahawia iliyokolea hadi nyekundu hupatikana kwenye majani (mara nyingi kando ya mshipa mkuu), vitawi vidogo, matawi, na matunda. Wadudu gamba hawa huonekana kama madoa yaliyoinuka yakiwa na umbo la pia huku sehemu ya kati ikionekana wazi zaidi (umbile kama la volkano). Duara la mwanga wa manjano linaweza kuonekana kuzunguka doa sehemu wanayokula. Wakati wa mashambulizi makali, majani hunyauka, kudondoka kabla ya wakati, na kupukutika kwa majani hutokea. Vitawi vilivyoathirika vitakufa, na hali hii inaweza kuenea hadi kwenye matawi makubwa endapo maambukizi ni makubwa. Matunda yanaweza kufunikwa na magamba kadhaa, kuharibika umbo, na hatimaye kukauka na kudondoka chini. Miti michanga inaweza kudumaa vibaya sana au hata kufa ikiwa matawi mengi yanadhohofika. Mdudu gamba mwekundu pia hutoa maji maji/umande wa asali ambao unaweza kusababisha kutokea kwa ukungu ulio mithili ya masizi kwenye majani na matunda.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Maadui wa asili wa wadudu gamba wekundu ni pamoja na nyigu-vidusia aina ya Aphytis melinus na Comperiella bifasciata, na utitiri wa wawindaji Hemisarcoptes malus ambao hushambulia wadudu gamba wachanga (watambaaji). Udhibiti wa maji moto ni muhimu katika udhibiti wa kibaiolojia kwa sababu maji moto hutoa ulinzi kwa wadudu gamba dhidi ya maadui wa asili. Upuliziaji wa mafuta ya petroli ya kikaboni yaliyoidhinishwa inaweza pia kutumika kuondoa wadudu gamba kwenye majani na matunda. Baada ya mavuno, safisha matunda ili kuondoa magamba kwenye matunda yako.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi kwa kuchukua hatua za kinga pamoja na udhibiti wa kibaiolojia, ikiwa unapatikana. Upuliziaji wa mafuta yaliyochujwa/kusafisha kwa kiwango kikubwa una athari ndogo kwa maadui wa asili wa wadudu hawa na inakuwa bora zaidi upuliziaji ukifanyika katikati ya majira ya joto. Upuliziaji wa kemikali za kupunguza makali ya dalili unapaswa kufanyika wakati zaidi ya 25% ya matunda yameathirika. Tumia dawa za kuua wadudu kwa kuchagua sehemu za shamba ambazo idadi ya wadudu gamba wekundu inazidi kiwango hiki. Epuka kutumia madawa yanayoua aina mbalimbali za wadudu kwa sababu yanaweza kuathiri hadi wadudu wenye manufaa ikiwamo maadui asili wa wadudu gamba.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na shughuli za ulaji kutoka kwa wadudu gamba wekundu wanaofahamika kitaalamu kama Aonidiella aurantii. Hii ni aina kuu ya wadudu waharibifu wa mimea jamii ya michungwa duniani kote, na ni wa kawaida zaidi katika maeneo ya tropiki. Baada ya mavuno wanakaa kwenye miti na majani, na kuwa tayari kushambuli ukuaji mpya katika msimu unaofuata. Wakati wa hatua yao ya kutembea, majike huvutiwa sana na mwangaza wakati wanapotafuta maeneo ya kula. Majike hawa hawatagi mayai bali huzaa wadudu watambaaji walio imara. Mara wanapotulia kwenye upande wa juu wa jani au kwenye matundu ya matunda machanga, katika hatua hiyo wanakuwa hawatembei. Baada ya hatua fupi ambapo hufunikwa na vitu mithili ya pamba, hatimaye hupata umbo lao la duara bapa na rangi yao ya kahawia nyekundu. Mzunguko wao wa maisha unahusiana kwa ukaribu na hali ya joto na afya ya miti. Hivyo basi, uharibifu mkubwa kwa kawaida hutokea mwishoni mwa majira ya joto, wakati ambapo miti inaweza kukumbwa na ukosefu wa unyevunyevu.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mitego ya harufu ili kuvutia majike na kutathmini ukali wa mashambulizi.
  • Kagua shamba lako mara kwa mara ili kubaini dalili za uwepo mdudu gamba na wakwangue ikiwa wapo kwa idadi ndogo.
  • Ondoa vitawi vidogo au matawi yaliyoathiriwa sana.
  • Punguza/pogoa matawi ili kuboresha mzunguko wa hewa kwenye mimea ili kutengeneza mazingira yasiyo rafiki kwa wadudu gamba.
  • Weka mitego au vizuizi vya kuwakamata au kuzuia maji moto wanaowalinda wadudu gamba dhidi ya maadui wake wa asili.
  • Epuka kutumia viuatilifu (dawa za kuua wadudu) vinavyoua aina nyingi za wadudu kwa sababu vinaweza kuathiri wadudu wenye manufaa (maadui wa mdudu gamba).
  • Punguza vumbi linalozingira majani na matunda kwa kunyunyizia maji barabarani na kuosha miti.

Pakua Plantix