Soya

Kiwavi-nywele Bihar

Spilarctia obliqua

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Kukauka kwa majani yaliyoambukizwa.
  • Kupukutika wa majani yote.
  • Majani yaliyounganishwa kwa wavu au utando.
  • Nondo wa kahawia wenye tumbo jekundu na madoa meusi.
  • Lava/viwavi waliofunikwa na nywele za njano hadi nyeusi.

Inaweza pia kupatikana kwenye

16 Mazao

Soya

Dalili

Majani yaliyoshambuliwa mapema huwa na rangi ya njano-kahawia na kukauka. Kadiri kiwavi anavyoendelea, tishu zote za jani huliwa. Chini ya shambulizi kali, mimea hupukutisha majani na shina pekee hubaki. Majani yanaonekana yakiwa yameunganishwa kwa wavu au utando na hatimaye kubaki na vishipa vitupu.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Idadi ya viwavi Bihar wenye manyoya kwa ujumla inaweza kudhibitiwa na maadui wengi wa asili hasa katika hatua ya lava wa S. obliqua. Vimelea wa manufaa ni vimelea wa braconid: Meteours spilosomae na Protapanteles obliquae, Glyptapanteles agamemnonis na Cotesia ruficrus pamoja na Ichneumonid Agathis sp. mbawakimia, mdudu kobe, buibui, mchwa mwekundu, kereng'ende, vunjajungu, mbawakawa wa ardhini, na mende wa ngao

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuua wadudu zinapaswa kushughulikiwa kwa tahadhari kwa sababu matumizi mengi ya viua wadudu yamesababisha spishi nyingi za nzi weupe kuwa sugu kwa dawa hizo. Ili kuzuia hili, hakikisha mzunguko sahihi kati ya viua wadudu na matumizi ya mchanganyiko. Nyunyizia Lambda-cyhalothrin 10 EC @ 0.6 ml/lita ya maji wakati viwavi wanapokuwa wachanga. Phenthoate 50% pia inachukuliwa kusaidia dhidi ya S. obliqua.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa zaidi na lava wa Spilarctia obliqua. Mdudu kamili ana sifa ya nondo wa kahawia wa ukubwa wa kati na tumbo jekundu na madoa meusi. Majike hutaga mayai yao (hadi 1000/jike) kwa makundi upande wa chini wa majani. Baada ya kuanguliwa, lava huwa na nywele ndefu za njano hadi nyeusi na hujigeuza kwa pupa kwenye takataka za majani karibu na mimea. Lava wakiwa kwenye hatua za mwanzo hula umbijani upande wa chini wa majani kwa wingi. Katika hatua za baadaye, lava hula majani kutokea kwenye kingo wakiwa mmoja mmoja. Kwa ujumla, lava hupendelea majani yaliyo komaa, lakini chini ya mashambulizi makali pia machipuki ya juu huathiriwa. Kiwavi Bihar mwenye manyoya hushambulia kunde, mbegu za mafuta, nafaka na baadhi ya mboga na jute katika nchi mbalimbali, na kusababisha uharibifu mkubwa wa kiuchumi. Kiwango cha upotevu wa mavuno hutofautiana kulingana na kiwango cha kushambuliwa na hali ya hewa kwani spishi hupendelea halijoto kutoka 18 hadi 33°C kwa ukuaji.


Hatua za Kuzuia

  • Panga kulima kwa kina majira ya kiangazi ili kuondoa udongo na kufichua pupa.
  • Epuka kupanda kabla ya monsuni(majira ya upepo mkali).
  • Tumia kiwango bora cha mbegu, sio zaidi au kidogo.
  • Nafasi ya kutosha kati ya mimea inapaswa kuzingatiwa.
  • Weka samadi iliyooza vizuri.
  • Panda mseto na mbaazi (zinazokomaa mapema), aina fulani za mahindi au mtama.
  • Fuatilia mashamba mara kwa mara ili uone dalili za wadudu (ukubwa wa mayai, viwavi na uharibifu wowote).
  • Tumia njia ifaayo ya palizi ama kwa dawa za kuulia magugu au kwa zana/mitambo shambani na maeneo ya kuzunguka.
  • Kusanya sehemu za mimea iliyoshambuliwa na kuiharibu mbali na shamba.
  • Jenga viunga na nafasi wazi kwajili ya kutua ndege ambao watakula viwavi.
  • Dhibiti matumizi ya viua wadudu vya wigo mpana, kwani hii inaweza kuathiri wadudu wenye faida.
  • Ondoa mabaki ya mimea au mimea ya kujiotea yenyewe baada ya kuvuna.
  • Fuata kwa mzunguko wa mazao ya yasiyo shambuliwa kama vile mpunga au mahindi.

Pakua Plantix