Karanga

Nondo wa Majani ya Karanga

Aproaerema modicella

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Majani yaliyo gugunwa/tobolewa kwenye sehemu za juu za majani.
  • Kutokea kwa madoa madogo ya kahawia kwenye majani.
  • Sehemu iliyoathiriwa zaidi, ukiwa kwa mbali huonekana kama imeungua.
  • Vipande vya majani hujikunja.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Karanga

Dalili

Majani yaliyo gugunwa/tobolewa na madoa madogo ya kahawia kwenye jani hutokea kutokana na kuliwa kwa ngozi ya juu ya jani. Lava huunganisha majani kwa utando na kuyala/kuguguna, huku wakibaki ndani ya mikunjo. Kwa mbali, maeneo yaliyoshambuliwa vikali huonekana kama yame chomwa moto. Kukauka kwa majani yaliyoathirika na kunyauka kwa mimea hutokea.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hifadhi idadi kubwa ya viumbe ambao ni maadui wa asili wa nondo wa majani; na maadui hawa ni kama vile buibui, panzi wenye pembe ndefu, vunjajungu, mchwa, mbawakavu mwenye madoa, nyenje, kati ya wengi. Panda mseto wa karanga na Pennisetum glaucum ili kuwezesha vimelea wanyonyaji wa Goniozus spp. kwa toboa toboa wa Majani ya Karanga.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia, ikiwa yanapatikana. Dawa za kikemikali za kunyunyizia zinapendekezwa tu wakati kuna angalau lava 5 kwa kila mmea katika hatua ya miche siku 30 baada ya kuota (DAE), au lava 10 katika hatua ya maua (siku 50 baada ya kutokea), na lava15 kwa kila mmea katika hatua ya kujaza maganda (Siku70 baada ya kutokea) kama wataonekana. Weka dawa ya kemikali yenye dimethoate katika 200-250 ml/ha (Chlorpyrifos @ 2.5 ml/l au Acephate @ 1.5 g/l) au Profenofos 20EC kwa 2 ml/lita kati ya siku 30-45 baada ya kupanda, ikiwa idadi ya wadudu ni juu ya Kiwango cha ukomo wa kiuchumi.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu wa karanga husababishwa na lava wa nondo wa majani ya maranga. Mayai ya nondo wa majani ya maranga yana rangi nyeupe inayong’aa na hutagwa moja kwa moja kwenye upande wa chini wa majani, huku lava/minyoo wakiwa na rangi ya kijani mpauko au kahawia wenye kichwa cheusi na kifua. Nondo wa Majani ya Karanga aliyekomaa ni nondo mdogo mwenye urefu wa milimita 6 hivi. Mabawa yake yana rangi ya kahawia-kijivu. Vijidoa vyeupe pia huwepo kwenye kila bawa la mbele la nondo wa majani ya karanga aliyekomaa. Lava/minyoo huguguna majani na kujilisha ndani yake. Hutoka nje ya mashimo waliyotoboa baada ya siku 5-6 na kuhamia kwenye majani ya karibu ili kula na kujigeuza mabuu/pupa kwenye majani yaliyo virigwa kwa utando. Maeneo yaliyotobolewa kwenye jani hukauka. Toboa toboa wa majani ya karanga huwa na uwezo wa kushambulia katika misimu yote ya mvua na baada ya mvua, na upotevu wa mazao unaweza kutofautiana kutoka 25% hadi 75%.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina ya mbegu ambazo ni sugu dhidi ya magonjwa, na mbegu hizi ni kama vile ICGV 87160 na NCAC 17090 ambazo zinaweza kutoa mavuno bora katika maeneo yenye nondo wengi wa majani ya karanga.
  • Panda mapema ili kuepuka mashambulizi ya baadae.
  • Panda mseto wa karanga na mazao ya mtego kama vile mtama wa lulu au kunde.
  • Tumia mitego ya mwanga kuvutia nondo nyakati za usiku, na kufuatilia idadi ya wadudu.
  • Ondoa mimea wenyeji mbadala kama vile soya na magugu kama lucerne, amaranthus, berseem na Indigofera hirsuta ili kudhibiti ukuaji wa wadudu.
  • Weka matandazo ya mabua ya mpunga ambayo husababisha kupungua kwa matukio ya toboa toboa wa majani ya karanga.
  • Fanya mzunguko wa mazao kwa kututumi mazao kama vile mahindi, pamba na mtama ili kutoa mazao bora na kupunguza matukio ya toboa toboa wa majani ya karanga.

Pakua Plantix