Mti wa jamii ya mchungwa

Usubi Mweusi wa Michungwa

Aleurocanthus woglumi

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Uwepo wa ute/umande wa asali kwenye majani na mashina.
  • Muonekano wa masizi.
  • Makundi ya uvimbe mdogo, mweusi kwenye upande wa chini ya jani.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mti wa jamii ya mchungwa

Dalili

Majani yaliyoathiriwa yanaweza kuonekana yamebadilika umbo na kupinda, na hatimaye kudondoka katika hatua ya awali za ukuaji. Ute wa asali unaonata hujikusanya kwenye majani na mashina, na kwa kawaida hutengeneza ukungu mweusi wa kuvu, na kusababisha muonekano wa masizi kwenye majani. Wadudu chungu wanaweza kuvutwa na ute wa asali. Wadudu hawa huonekana sana kama makundi ya uvimbe mdogo mweusi ulio mithili ya miiba kwenye sehemu ya chini ya majani. Mchanganyiko wa uharibifu unaotokana na kuliwa kwa sehemu za mmea na ukuaji wa ukungu wa masizi hudhoofisha miti na kupunguza uzalishaji wa matunda.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Vimelea vya Encarsia perplexa), Polaszek, na Amitus hesperidum silvestri vimebainika kuwa ni nyigu wa vimelea wa Usubi Weusi. Nyigu hawa wanafahamika kwa kuvamia usubi weusi wa machungwa pekee na pamoja na nzi weupe wanaofanana zaidi na usubi weusi, lakini hawadhuru mimea wala binadamu. Mbawakimia, mbawakimia wa kijani na jamii mbalimbali za wadudu-kibibi kama vile Brumus sp., Scymnus sp. and Chlysoperla sp. pia ni maadui wa asili wa Usubi Weusi wa Michungwa. Mafuta kama vile mafuta ya pamba na mafuta ya samaki na resini yanayofahamika kama Fish Oil Rosin Soap - FORS yana ufanisi katika kudhibiti usubi kibaiolojia na kwa asili ni rafiki kwa mazingira, siyo tu katika kupunguza idadi ya usubi weusi bali pia katika kupunguza ukungu wa masizi kwenye majani. Pulizia mvuke wa mbegu za mwarobaini (4%) ili kupunguza idadi ya wadudu hawa.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia, ikiwa yanapatikana. Epuka matumizi ya viuatilifu vinavyoua aina nyingi za wadudu ili kuhifadhi maadui wa asili (yaani wadudu wanaokula usubi weusi). Mdudu huyu anaweza kudhibitiwa kwa kufukiza (fumigation) vifaa vya kupanda au kwa kupulizia dawa za kemikali. Pulizia dawa za kuua wadudu za kutibu wakati zaidi ya 50% ya mayai yanapoanguliwa na vijidudu wachanga wakiwa hawana ngozi ngumu/gamba la kukinga kwenye miili yao. Dawa za kuua wadudu zinazofahamika kama Quinalphos zimeonekana kuwa na ufanisi katika kupunguza idadi ya usubi weusi. Upuliziaji lazima ufanyike kwenye upande wa chini wa majani ambako wadudu hawa hustawi. Taji lote la majani linapaswa kulowanishwa na mchanganyiko wa dawa.

Ni nini kilisababisha?

Usubi mweusi wa michungwa (kitaalamu Aleurocanthus woglumi) ni mdudu hatari kwa mimea jamii ya michungwa ambae asili yake ni bara la Asia na hushambulia aina mbalimbali za mimea wanamoweza kuishi. Wadudu hawa ni sehemu ya familia ya nzi weupe, lakini usubi kamili wana mwonekano wa rangi ya giza, buluu ya kijivu, hali iliyompa jina la usubi mweusu. Usubi kamili ni mdogo sana, goi goi na asiye na uwezo wa kuruka mbali, lakini huwa mwenye hekaheka wakati wa jioni na mchana hupumzika kwenye sehemu ya chini ya majani. Majike huzalisha takriban mayai 100 yenye rangi ya dhahabu, ambayo huyataga kwenye mpangilio wa mzunguko (mithili ya spiringi) kwenye sehemu ya chini ya majani. Vijidudu wachanga wanakuwa bapa, umbo la yai, na mwonekano wa mithili ya magamba. Utomvu/majimaji ya seli hufyonzwa kutoka kwenye majani kupitia mdomo wa usubi mweusi unaodunga mithili ya mwiba. Wakati huohuo, usubi hutoa ute wa asali kwa kiwango kikubwa. Hali muafaka kwa ukuaji wa usubi mweusi ni joto la takriban 28-32°C na unyevunyevu wa asilimia 70-80%. Usubi hawa hawezi kuishi katika mazingira ya baridi kali ambapo barafu hutokea.


Hatua za Kuzuia

  • Hakikisha unatumia mimea isiyo na wadudu waharibifu kwenye shamba lako.
  • Tengeneza mazingira mazuri ya mzunguko wa hewa kwenye shamba lako kwa kuepuka kupanda kwa kukaribiana.
  • Kupogoa vizuri na kuondoa mimea mbadala inayohifadhi vimelea (magugu na mazao mengine wenyeji) kutapunguza maeneo pendwa ya usubi mweusi.
  • Fuatilia miti yako mara kwa mara ili kubaini dalili za uwepo wa wadudu waharibifu na sehemu za mimea zilizoathiriwa na masizi.
  • Mwagilia maji ya kutosha na mbolea ya kiasi, lakini epuka hali ya kutuamisha maji au hali ya kimazingira isiyo rafiki kwa mimea ili kudumisha afya ya miti yako ya jamii ya machungwa.
  • Epuka umwagiliaji kupita kiasi na matumizi ya naitrojeni pamoja na upuliziaji wa dawa za kuua wadudu.
  • Ondoa mabaki yoyote yanayoweza kubeba wadudu msimu wa baridi ili kupunguza nafasi ya maambukizi mapya msimu ujao wa ukuaji.

Pakua Plantix