Papilio demoleus
Mdudu
Majani machanga huliwa kuelekea ndani kutokea kwenye kingo za majani. Majani yanaweza kuliwa kabisa, na kusababisha kupukutika kwa majani ya kwenye vitawi. Kipepeo mdogo na mkubwa wa machungwa anaweza kuondoa majani kutoka kwenye miti ya machungwa na kutoa harufu kali wanaposumbuliwa.
Mayai ya kipepeo cha machungwa hushambuliwa na spishi kadhaa za wadudu wa Ooencyrtus, na lava hushambuliwa na Apanteles pallidocinctus Gahan. Katika Hatua ya pupa pia hushambuliwa na vijidudud aina ya Pteromalus puparum L.
Pulizia Fenithrothion mara 2-3 kwa vipindi vya siku 15. Matibabu ya shina kwa kutumia Azodrin yana sumu kwa lava au mabuu wa kipepeo cha machungwa wenye urefu wa chini ya 10 mm. Matibabu ya shina kwa kutumia Citrimet yana ufanisi katika kulinda miti michanga. Matibabu ya kupulizia kama Dipel 2x, Thuricide, Lannate SL, n.k. yanaweza kutumika kama kipulizio cha nje cha kulinda majani.
Husababishwa na viwavi wa kipepeo anaeshambulia mimea ya jamii machungwa. Viwavi hula majani machanga katika hatua ya kitalu na pia kwenye ukuaji wa majani machanga ya miti iliyokomaa. Viwavi waliokomaa wana rangi ya kijani. Maambukizi makubwa husababisha mti mzima kupukutisha majani.