Mti wa jamii ya mchungwa

Lusina wa Michungwa

Diaphorina citri

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Lusina wakubwa na tunutu hufyonza utomvu kutoka kwenye machipukizi machanga, na hivyo kusababisha uharibifu na udhoofu wa machipukizi, maua, mashina laini, na matunda madogo.
  • Majani hufunikwa na umande wa asali na ukungu wa masizi, maua machanga na matunda hudondoka.
  • Vitawi hukauka endapo mashambulizi ni makubwa.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mti wa jamii ya mchungwa

Dalili

Lusina wa michungwa huathiri miti ya jamii ya michungwa kwa njia tofauti, kutegemea na hatua ya ukuaji na muda wa msimu. Ulaji wa lusina kamili na tunutu (lusina wachanga) unaweza kuharibu na kudhoofisha kuchipuka, kama vile machipukizi, maua, vishina laini, na matunda madogo. Uwingi wa umande wa asali unaozalishwa wakati wa kufyonza utomvu wenye sukari husababisha ukuaji wa ukungu mweusi na kupunguza shughuli za usanidimwanga kwenye majani. Mwishowe, katika hali ya uwepo wa idadi kubwa ya wadudu hawa, kujikunja na kujisokota kwa majani mapya, na kupungua kwa urefu wa vishina, hali hiyo mara nyingi husababisha hali inayojulikana kama athari ya shada la kichawi; hali ambayo vishina, vitawi na majani huchomoza kutokea sehemu moja na kutengeneza kitu mithili ya kichaka. Idadi kubwa ya lusina hudumaza ukuaji wa miti michanga na husababisha upungufu mkubwa wa mavuno. Wadudu hawa wanaweza kuwa hatari sana kwa sababu pia ni waenezaji wakuu wa ugonjwa kijani kibichi.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Wadudu wanaokula wadudu waharibifu pamoja na vimelea wana uwezekano mkubwa wa kutoa udhibiti endelevu wakati kuna idadi ndogo ya lusina, kwa mfano wakati wa hali ya hewa ya joto na ukavu. Nyigu wa vimelea ni pamoja na nyigu vidusia au nyigu wanaofahamika kitaalamu kama Psyllaephagus euphyllurae. Wadudu wanaokula wadudu wengine ni pamoja na mdudu haramia, mbawakimia, na mdudu-kibibi. Sabuni za kuua wadudu zinazotokana na mafuta ya mwarobaini au mafuta yanayotokana na mbogamboga pia yanafaa kudhibiti idadi ya wadudu, lakini zinapaswa kutumika kabla tunutu hawajazalisha nta yao ya kujikinga.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na tiba za kibaolojia ikiwa zinapatikana. Kupulizia kwa wakati dawa za kuua wadudu zinazotokana na dimethoate, imeonesha kuwa na ufanisi dhidi ya lusina, lakini zinapaswa kutumika kama chaguo la mwisho. Dawa hizi zinapaswa kupuliziwa kabla ya wadudu hawa hawajatoa nta ya ulinzi, ambayo huwapatia ukinzani wa kiasi fulani. Kumbuka kuwa matumizi ya kupita kiasi ya dawa hii yanaweza kusababisha kuongezeka tena kwa lusina wa michungwa na wadudu wengine. Magamba ya mti yanaweza kutibiwa kwa dawa ya dimethoate (0.03%) ili kuwaangamiza wadudu wanaohama kwa kupanda juu na kushuka chini ya mti.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na shughuli za ulaji za lusina wa michungwa, Lusina wa Machungwa wa Asia. Lusina kamili wana urefu wa milimita 3 hadi 4, na vichwa na vifua vyenye rangi ya kahawia nyeusi, na matumbo ya kahawia iliyofifia pamoja na mbawa zenye madoa. Wadudu hawa wanaweza kuishi msimu wote wa baridi katika maeneo yenye kivuli kwenye shina au kwenye majani yaliyokomaa. Wastani wa muda wa maisha ya lusina kamili hutegemea joto, ambapo nyuzi joto 20-30 °C ndio bora zaidi. Hali ya hewa ya baridi huongeza muda wao wa kuishi, ilhali hali ya joto kali hupunguza. Majike wana uwezo wa kutaga hadi mayai 800 ya rangi ya machungwa kwenye vishina vipya na machipukizi wakati wa majira ya kuchipua. Tunutu wanakuwa bapa, kwa kawaida wakiwa na rangi ya manjano, na huzalisha utando mweupe wenye nta ambayo huwakinga. Ukuaji wa nta mweupe au nyuzi huwafanya watofautiane wazi na vidukari. Ikilinganishwa na wadudu kamili, tunutu hutembea kwa umbali mfupi tu ikiwa watasumbuliwa. Uharibifu kwa tishu za mimea huathiri uwezo wa mmea kusambaza virutubisho kwenye sehemu zote.


Hatua za Kuzuia

  • Fuatilia mimea mara kwa mara ili kubaini dalili za uwepo wa lusina, kuanzia mwanzoni mwa msimu wa kuchipua.
  • Tumia mitego yenye gundi kama inavyopendekezwa ili kuwanasa lusina kamili.
  • Acha nafasi ya kutosha kati ya miti wakati wa kupanda.
  • Hakikisha kuwa hutumii kwa kiwango kikubwa dawa za kuua aina mbalimbali za wadudu ili kuepuka kuathiri idadi ya wadudu wanaokula lusina wa michungwa.
  • Hakikisha kuna mzunguko wa kutosha wa hewa kwenye majani pamoja na mwangaza wa kutosha wa jua, ili kutengeneza mazingira yasiyo rafiki kwa lusina.
  • Epuka matumizi ya mbolea kupita kiasi wakati wa msimu.
  • Mwagilia mashamba ya matunda mara kwa mara wakati wa msimu wa ukame ili kuepuka mimea kuathiriwa na ukame.
  • Safisha mashamba ya matunda kwa kuondoa matawi ya zamani na mabaki baada ya mavuno.

Pakua Plantix