Muwa

Panzi-vidukari wa Miwa

Pyrilla perpusilla

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Wadudu wa kijani hadi kahawia hula upande wa chini wa majani.
  • Majani kuwa ya njano na kukauka, mimea iliyodumaa.
  • Uzalishaji wa umande wa asali na ukuaji wa ukungu wa masizi kwenye uso wa majani.
  • Tofauti na mahindi, wadudu hawa pia hushambulia kwa urahisi nyasi na nafaka nyingine.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Muwa

Dalili

Mdudu huyu hupatikana sehemu ya chini ya majani ambapo hufyonza utomvu wa mmea. Hii husababisha rangi ya njano kwanza na kisha kukauka kwa majani. Chini ya uvamizi mdogo, mabaka ya manjano yanaonekana kwenye uso wa jani. Usanisinuru hupungua na kusababisha kudumaa kwa mmea. Wadudu hawa warukao pia hutoa dutu tamu inayoitwa umande-asali ambayo hufunika majani. Hii huvutia fangasi nyemelezi ambao ukuaji wao unafanya jani kuwa jeusi. Hii inapunguza usanisinuru zaidi na zaidi, na kusababisha hasara ya mavuno. Mbali na mahindi, wadudu hawa pia hushambulia kwa urahisi miwa, ulezi, mpunga, shayiri, oti, mtama, bajra na nyasi mwitu.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Vidusia kadhaa hushambulia mayai na tunutu. Vidusia wa mayai ni pamoja na Tetrastichus pyrillae, Cheiloneurus pyrillae, Ooencyrtus pyrillae, O. pipilionus na Agoniaspis pyrillae. Tunutu hushambuliwa na Lestodryinus pyrillae, Pyrilloxenos ompactus, Chlorodryinus pallidus, Epiricania melanoleuca. Wawindaji wa wadudu hawa pia hujumuisha aina kadhaa za mdudu kobe kama vile Coccinella septempunctata, C. undecimpunctata, Chilomenes sexmaculata, Brumus suturalis. Washambuliaji wa mayai ni Nimboa basipunctata, Goniopteryx pusana.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Bidhaa zenye Chlorpyriphos zinafaa dhidi ya wadudu hawa.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na wadudu wakubwa wa Pyrilla perpusilla, mdudu ambae ni amilifu sana anae zaliana mwaka mzima na huweza kuhama kutoka shamba hadi shamba, na kusababisha uharibifu mkubwa. Wadudu wakubwa ni kijani hadi rangi ya majani makavu na urefu wa 7-8 mm. Kwa kawaida hupatikana wakila mimea kwa wingi na huruka kwa urahisi wanapovurugwa. Pua yao iliyochongoka huficha sehemu za mdomo ambazo hutoboa na kunyonya tishu za mmea. Kuenea kwa wadudu husaidiwa na unyevu wa juu na ukuaji wa haraka wa mimea, kwa mfano katika mashamba yenye samadi nyingi au mbolea. Umwagiliaji kupita kiasi au msimu wa mvua pia huchangia ueneaji wake.


Hatua za Kuzuia

  • Fuatilia shamba mara kwa mara kwa dalili za wadudu.
  • Ondoa mmea ulioambukizwa baada ya kuvuna na uchome moto.
  • Usitumie viua wadudu vya wigo mpana kwani hivi vinaweza kuathiri vibaya wadudu wenye faida.

Pakua Plantix