Bamia

Kidusufi wa Pamba

Oxycarenus hyalinipennis

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Nyuzinyuzi zilizochafuka na kudondoka kwa vitumba.
  • Kubadilika rangi kwa vitumba vya pamba.
  • Mbegu nyepesi ambazo hazijakua vizuri.
  • Mabuu hubadilisha rangi yao kutoka rangi ya waridi hadi kahawia.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Bamia

Dalili

Pia hujulikana kama mdudu mchafua pamba, mdudu huyu na tunutu wake hushambulia hasa vitumba vya pamba ambavyo vimefunguka kwa kiasi, na hivyo kusababisha nyuzi za pamba kuchafuka, vitumba kubadilika rangi, kuoza, na wakati mwingine kudondoka (kwa kiasi fulani, kutokana na bakteria wanaoenezwa wanapokula utomvu wa pamba). Dalili zaidi ni mbegu ambazo hazijakua vizuri, nyepesi, ambazo hushindwa kuiva ipasavyo. Mashambulizi makubwa yanaweza kusababisha upotevu mkubwa wa ubora wa mavuno kwa sababu ya pamba iliyochafuliwa, hivyo jina maarufu kuwa mdudu mchafua pamba. Wadudu hawa wanapokula mimea mingine mbadala inayowawezesha kuishi kama vile bamia, dalili za kawaida ni harufu kali na utokaji wa vitu mithili ya grisi.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Barani Afrika, baadhi ya vimelea vya utitiri hupatikana kwenye wadudu hawa, ambao hatimae huwa legevu na kufa mapema. Baadhi ya buibui pia hushambulia mdudu huyu. Dawa za kupulizia majani zenye mafuta yaliyozimuliwa ya mwarobaini (5%), Kuvu Kiuawadudu, kama vile Beauveria bassiana na Metarhizium anisopliae pia zimeonyesha athari kiasi katika kudhibiti idadi ya vidusufi.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zikiwa na hatua za kuzuia na matibabu ya kibaolojia, ikiwa yapo. Kupulizia majani kwa dawa za kuua wadudu zenye chlorpyrifos, esfenvalerate, bifenthrin, deltamethrin, lambda-cyhalothrin, au indoxacarb ni hatua inayofanya kazi dhidi ya funza wa vitumba wa pinki(pink bollworm) na imeonesha kupunguza idadi ya vidusufi wa pamba. Hata hivyo, kwavile mdudu huyu mara nyingi hushambulia mashamba mwishoni mwa msimu, udhibiti wa kikemikali mara nyingi hauwezekani kutokana na mabaki kwenye mavuno. Vilevile kuna taarifa za usugu dhidi ya dawa za kuua wadudu.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na kidusufi ambae kitaalamu anafahamika kama Oxycarenus hyalinipennis. Huyu ni mdudu anayekula aina nyingi za mimea ambae pia anaweza kuwa mdudu hatari kwa pamba. Vidusufi waliokomaa hufikia urefu wa milimita 4-5 na wana rangi ya kahawia iliyo kolea na mbawa angavu. Madume ni wadogo kidogo kuliko majike. Mayai yenye rangi mithili ya nyeupe mchanganyiko na manjano hutagwa kwa makundi ya hadi mayai manne kwenye nyuzinyuzi za vitumba vilivyo wazi, karibu na mbegu. Tunutu hufikia urefu wa milimita 2.5 na hubadilika rangi zao kutoka rangi ya waridi (pinki) hadi kahawia wakati wa hatua tofauti za mzunguko wa maisha yao, ambao hudumu kwa jumla ya takribani siku 40-50. Shambulio hutokea mwishoni mwa msimu, wakati vitumba vingi vikiwa vimefunguka tayari. Mimea mingine inayohifadhi vidusufi ni pamoja na bamia na mimea mingine ya familia ya malvaceae.


Hatua za Kuzuia

  • Kagua mashamba na angalia uwezekano wa uwepo wa wadudu wadogo ndani na kuzunguka vitumba vya pamba vilivyo wazi.
  • Ondoa wadudu kwa mikono ikiwa idadi yao ni ndogo.
  • Vinginevyo, weka mitego ya mwanga wa UV katika maeneo ambayo pamba au bamia hulimwa.
  • Ondoa mimea mbadala inayohifadhi wadudu ambayo ipo kwenye shamba au kuzunguka shamba.

Pakua Plantix