Soya

Mbawakavu wa Mkole wa Soya

Obereopsis brevis

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Mikato miwili ya mduara kwenye tawi au shina.
  • Kuanguka na kukauka kwa majani.
  • Kunyauka na kufa kwa mimea mchanga.
  • Mbawakavu ana kichwa na kifua cha rangi ya nyekundu-njano, vifuniko vya mabawa vya kahawia.
  • Lava huonekana weupe wenye kichwa cheusi.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Soya

Dalili

Dalili za wazi zinaweza kuonekana katika hatua ya miche zenye sifa ya mikato ya mduara kwenye tawi la mmea au shina. Miche na mimea michanga hunyauka au kufa wakati majani ya mimea ya zamani hunyauka tu au kuwa kahawia, na yote hukauka. Pete za duara zitaonekana kwenye matawi yaliyoathirika. Sehemu iliyoshambuliwa juu ya mkato hatimaye hukauka. Katika hatua ya baadaye ya mashambulizi, mmea hukatwa kwa umbali wa cm 15 - 25 juu ya ardhi.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hadi leo, hakuna matibabu ya asili yenye ufanisi. Chaguzi mbadala za udhibiti wa mbawakavu wa soya hutegemea matumizi ya hatua za kuzuia na za kitamaduni.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia, ikiwa yanapatikana. Ikiwa uharibifu unazidi kizingiti cha kiuchumi cha 5%, unaweza kutumia NSKE 5% au azadirachtin 10000 ppm @ 1 ml/1 l ya maji ili kuzuia mbawakavu wa kizingo kutaga mayai. Cartap hydrochloride granular kilo 4 kwa ekari inaweza kusambazwa wakati wa kupanda. Nyunyizia Lambda-cyhalothrin 5 EC @ 10 ml au Dimethoate 25 EC @ 2 ml kwa lita ya maji katika siku 30 - 35 baada ya kupanda na kurudia utaratibu siku 15 - 20 baada ya unyunyiziaji wa mwanzo, ikiwa maambukizi yameonekana. Chlorantraniliprole 18.5% SC @ 150 ml/ha, Profenophos na Trizophos pia hupendekezwa katika hatua ya kuchipua au kutoa maua.

Ni nini kilisababisha?

Dalili hizo husababishwa zaidi na lava weupe, wenye mwili laini na wenye vichwa vyeusi wa Oberopsis brevis. Mbawakavu walio komaa wana sifa ya rangi ya nyekundu-manjano kwenye kichwa na kifua, na magamba ya rangi ya kahawia ya elytra (vifuniko vya mabawa). Mayai hutagwa katikati ya mikanda na majike. Lava watatoboa kwenye shina na kula kwa ndani, na kutengeneza handaki kwenye shina. Sehemu iliyoshambuliwa juu ya mkato haiwezi kupata lishe ya kutosha na hukauka. Hasara kubwa ya mavuno hutokea hatimaye. Hali ya hewa inayofaa kwa mbawakavu ni joto kati ya 24 - 31 ° C na unyevu wa juu wa anga.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina zinazostahimili, kama vile NRC-12 au NRC-7.
  • Tawanya mbegu sawasawa wakati wa kupanda kwa wakati unaofaa (yaani mwanzoni mwa monsuni).
  • Epuka matumizi mengi ya mbolea ya naitrojeni.
  • Kusanya na kuharibu sehemu za mmea zilizoshambuliwa angalau mara moja kila baada ya siku 10.
  • Baada ya kuvuna, haribu mabaki ya mazao.
  • Mzunguko wa mazao unapendekezwa, lakini epuka kupanda mseto na mahindi au mtama.
  • Tayarisha udongo kwa msimu ujao kwa kulima kwa kina katika miezi ya kiangazi.
  • Shaincha inaweza kutumika kama zao la mtego.

Pakua Plantix