Dysdercus cingulatus
Mdudu
Wadudu kamili (wakubwa) na tunutu (wadudu wachanga) hula kwenye vitumba vya maua na kwenye vitumba vya pamba ambavyo havijafunguka kabisa au vilivyofunguka nusu. Wadudu hawa huchimba kupitia nyuzi na kula mbegu. Tishu zilizoharibiwa hukaliwa na vijidudu vinavyosababisha kuoza kwa vitumba vya pamba na kubadilika rangi. Kudondoka kwa vitumba, kufunguka mapema (kabla ya wakati), na kudondoka mimea mapema ni hali za kawaida. Dalili nyingine ni mbegu ndogo zenye kiwango kidogo cha mafuta, nyuzi zilizochafuka, na kiwango cha chini cha uotaji. Mbegu hizi hazifai kupandwa. Mdudu huyu hategemei mmea mmoja na anaweza kuhamia kwenye vitumba vingine vichanga. Uvamizi mkubwa wa wadudu unaweza kusababisha upotevu mkubwa wa ubora wa pamba kutokana na nyuzi zilizochafuka.
Kupulizia majani kwa mafuta ya mwarobaini yaliyozimuliwa imeonekana kuwa na ufanisi dhidi ya mdudu huyu.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia na tiba za kibaiolojia endapo zinapatikana. Upuliziaji majani kwa dawa za kuua wadudu zenye chlorpyrifos, esfenvalerate, au indoxacarb hufanya kazi dhidi ya funza wa vitumba na pia imeonyesha uwezo wa kupunguza idadi ya wadudu wekundu wa pamba. Hata hivyo, kwa suala la uvamizi wa kuchelewa, udhibiti wa kikemikali mara nyingi unakuwa hauna ufanisi kwa sababu ya mabaki yaliyopo kwenye vitumba wakati wa mavuno.
Uharibifu unasababishwa na tunutu (vidusufi wachanga) na vidusufi kamili (wakubwa/waliopevuka) waitwao Dysdercus cingulatus. Wadudu wakubwa wanaweza kufikia urefu wa milimita 12-13 na wana rangi ya kipekee ya nyekundu-machungwa. Kichwa ni chekundu kikiwa na kola nyeupe, fumbatio (tumbo) ni jeusi na mbawa za mbele zina madoa mawili meusi. Madume ni madogo kuliko majike. Majike yanaweza kutaga hadi mayai 130 yenye rangi ya njano angavu kwa wakati mmoja kwenye udongo, karibu na mimea mbadala inayohifadhi vijidudu. Baada ya kipindi cha kuatamia cha siku 7-8, tunutu huanguliwa na kuanza kula mimea ya pamba. Na wenyewe pia ni wekundu na wana madoa matatu meusi kwenye fumbatio na jozi tatu za madoa meupe mgongoni. Kipindi cha ukuaji huchukua jumla ya siku 50-90, kutegemea na hali ya hewa. Uvamizi hutokea kuelekea mwishoni mwa msimu, wakati vitumba vya kwanza vinapofunguka. Mimea mbadala inayohifadhi vijidudu vya vidusufi ni pamoja na bamia, haibiskasi, na mimea jamii ya michungwa.