Mzeituni

Kunguni Lesi wa Mzeituni

Froggattia olivinia

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Kubadilika rangi kwa madoadoa kwenye uso wa jani.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Mzeituni

Mzeituni

Dalili

Madoadoa ya njano yasiyo na mpangilio (kubadilika rangi kwa madoadoa) kwenye uso wa jani ambayo hubadilika kuwa kahawia na hatimaye majani kudondoka. Uharibifu husababisha upukutishaji mkubwa wa majani na kupunguza mavuno ya matunda.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Kwa kiwango kidogo, udhibiti wa kibiolojia unaweza kufanikiwa. Kunguni lesi wanaripotiwa kuwa na vimelea vya mayai lakini hii haina uwezekano wa kuwepo katika mashamba mengi ya mizeituni ya kawaida, hasa kama ardhi ni wazi (vimelea wa mayai kwa kawaida hula nekta). Mbawa chekeche wa kijani ni mdudu mla wadudu anae tumiwa sana kwa udhibiti wenye mafanikio.

Udhibiti wa Kemikali

Ni rahisi kuwaua kunguni lesi ikiwa sehemu zote za majani zitafikiwa na viua wadudu vya kemikali wakati wa kunyunyizia. Pareto ya asili (pyrethrin) na pareto ya kiwandani (pyrethroids) ni bora katika kudhibiti kunguni lesi wa mzeituni. Chumvi za potasiamu ya asidi ya mafuta, pia hujulikana kama chumvi za sabuni, zimeripotiwa kudhibiti wadudu hawa. Baadhi ya organophosphates zinaweza kutumika katika kiwango cha uzalishaji. Rudia dawa kwa mara ya pili ili kudhibiti tunutu wapya walioanguliwa baada ya siku 10-14. Unapotumia dawa, vaa nguo za kujikinga kila wakati na ufuate maagizo yaliyo kwenye lebo ya bidhaa, kama vile kipimo, muda wa matumizi, na muda wa kabla ya kuvuna. Daima fuata kanuni za ndani za matumizi ya dawa.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na Froggattia olivinia. Ni kawaida kuona hatua tofauti za wadudu waliokusanyika upande wa chini wa majani yaliyo haribiwa. Mayai ambayo yalisalia kwenye mti kwa msimu wote wa baridi kawaida huanza kuangua wakati wa majira ya kuchipua au mwishoni mwa msimu wa baridi. Wadudu walikomaa wanaweza kuruka umbali mfupi. Ulaji wa wadudu wachanga na waliokomaa husababisha madoadoa ya njano yasiyo na mpangilio kwenye uso wa majani. Kunguni kitani wa mizeituni anaweza kuwa na vizazi vingi kwa mwaka kulingana na hali ya hewa. Maambukizi mapya yanaweza kutokea mara kwa mara katika msimu wa ukuaji. Hatua zote ambazo wadudu wa uwezo wa kutembea zina sehemu wana sehemu za mdomo za kutobolea na kunyonya, kwa hivyo hatua zote husababisha uharibifu.


Hatua za Kuzuia

  • Fuatilia miti yako mwanzoni mwa majira ya kuchipua kujua dalili za kushambuliwa na wadudu.
  • Tekeleza hatua za udhibiti mara tu unapogundua uwepo wa dalili za wadudu(kunguni).
  • Idadi ya kunguni kitani inaweza kuongezeka haraka ikiwa haitadhibitiwa.
  • Pogoa miti iliyoshambuliwa vibaya ili kurahisisha njia za kudhibiti.
  • Kupogoa pia kutasaidia kurejesha(kuifanya upya) miti iliyoharibiwa vibaya.
  • Ufuatiliaji wa mara kwa mara wa wadudu unahitajika kila baada ya wiki mbili katika msimu mzima wa ukuaji, haswa baada ya kushambuliwa kwa mara ya kwanza katika msimu huo huo.
  • Zingatia sana ukingo wa shamba kwani idadi ya watu inaweza kusonga na kuhamia upande mwingine.

Pakua Plantix