Mbiringanya

Kipekecha Shina na Tunda la Biringanya

Leucinodes orbonalis

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Alama za kula kwenye maua na vitumba.
  • Kunyauka kwa ncha za mfumo wa shina (kama vile vitawi, majani, machipukizi, n.k) na shina kuu.
  • Mashimo ya kuingilia na kutokea yanazibwa na kinyesi kikavu kwenye matunda.
  • Matunda yaliyotobolewa yamejaa kinyesi.
  • Lava ni wa rangi ya pinki wakiwa na kichwa chenye rangi ya kahawia.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mbiringanya

Dalili

Dalili ya kwanza kuonekana ni kunyauka kwa ncha za shina kutokana na kuliwa mapema na lava. Baadaye, maua, vitumba vya maua, na shina pia huathirika. Lava wachanga hutoboa sehemu ya mwisho ya mshipa wa kati (vena kuu) wa majani makubwa na vishina laini ili kujipenyeza kwenye shina na kusababisha kudumaa. Lava waliopevuka hutoboa matunda na kuacha mashimo madogo ya kuingilia yakiwa yamezibwa na kinyesi kilichokauka. Ndani ya tunda kunakuwa na uwazi wenye rangi isiyo ya kawaida huku ukiwa umejaa kinyesi cha lava. Kunyauka na kudhoofika kwa mimea kunaweza kutokea wakati wa uvamizi mkubwa wa lava, na kusababisha upotevu wa mavuno. Matunda yanayotokana na mimea iliyoathirika yanaweza kuwa yasifae kwa matumizi. Uharibifu unakuwa mbaya zaidi wakati idadi kubwa ya wadudu inajijenga kwa vizazi kadhaa.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Vijidudu mbalimbali hula lava wanaooneza ugonjwa huu, kwa mfano, Pristomerus testaceus, Cremastus flavoorbitalis, na Shirakia schoenobic. Spishi za Pseudoperichaeta, Braconids, na Phanerotoma pia zinapaswa kuimarishwa au zinaweza kuingizwa kwenye shamba. Mchanganyiko wa mbegu za mwarobaini kwa asilimia 5 au spinosad unaweza pia kutumika kwenye matunda yaliyoshambuliwa. Nyavu au chandarua zenye gundi zinaweza kutumika juu ya ukingo wa sentimita 10 ili kuzuia mayai kutagwa. Ikiwa gundi haipatikani, refusha nyavu au chandarua hizo sentimita 40 juu ya urefu wa mita 2 kwenda juu, kisha teremsha chini kwenye pembe ya nyuzi 80-85 dhidi ya chandarua kilicho wima.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi ikiwa na hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa inapatikana. Matibabu yatatofautiana kutegemea na hatua ya maambukizi na msimu. Kupulizia sevimol (0.1%) kwa vipindi vya kawaida husaidia kudhibiti kuenea kwa wadudu. Epuka matumizi ya dawa za pyrethroids na matumizi ya dawa za kuua wadudu wakati wa matunda kukomaa na wajati wa mavuno.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu unasababsishwa na lava wa wa nondo anayefahamika kitaalamu kama Leucinodes orbonalis. Katika majira ya kuchipua, majike hutaga mayai yenye mchanganyiko wa rangi nyeupe na malai (krimu). Majike hutaga mayai moja moja peke yake au kwa vikundi upande wa chini wa majani, kwenye shina, vitumba vya maua, au kwenye kitako cha tunda. Lava huangua mayai baada ya siku 3 hadi 5 na kwa kawaida huchimba mashimo moja kwa moja kwenye tunda. Lava aliyepevuka anakuwa mwenye nguvu, rangi ya pinki na kichwa cha kahawia. Lava wakishamaliza kula, mabadiliko yao hutokea kwenye kifuko cha kijivu kilicho imara huku kikiwa kimefumiwa kwenye shina, vishina vilivyokauka, au miongoni mwa majani yaliyanguka. Hatua ya pupa inachukua siku 6 hadi 8, baada ya hapo nondo kamili hutokea. Nondo huishi kwa siku mbili hadi tano, wakikamilisha mzunguko wa maisha unaodumu siku 21-43 kutegemea na hali ya mazingira. Kunaweza kuwa na hadi vizazi vitano vinavyopishana kwa mwaka wa uhai wao. Wakati wa baridi, lava hujificha ndani ya udongo. Wadudu huu hula mimea mingine mingi ya jamii ya solanaceous kama vile nyanya na viazi.


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina za mimea yenye ukinzani au zinazostahimili magonjwa, ikiwa zinapatikana katika eneo lako.
  • Ikiwa inawezekana, changanya kwa misimu miwili mimea inayoweza kuhifadhi vimelea vya magonjwa pamoja na mimea ya jamii zingene kama vile shamari ( kiungo jamii ya karoti), omum (ajwain), giligilani (coriander) na nigella.
  • Fuatilia kwa ukaribu eneo la kilimo mara kwa mara ili kugundua uwepo wa dalili za vimelea.
  • Majani, sehemu za shina, au matunda yaliyoathirika vinapaswa kuondolewa na kuharibiwa mbali na shamba.
  • Hakikisha ardhi inakuwa safi kutoka kwenye matunda, majani na vishina vilivyoanguka.
  • Iwapo kuna uvamizi mkubwa wa wadudu, mmea mzima unapaswa kung'olewa na kuharibiwa.
  • Tumia chandarua za nailoni kama vizuizi vya kuzuia kuhama kwa nondo kwenda kwenye mazao au mashamba mengine.
  • Tumia mtego wa feromoni ili kuvutia au kukamata nondo kwa wingi.

Pakua Plantix