Cryptomyzus ribis
Mdudu
Malenge lenge makubwa yenye rangi nyekundu hadi zambarau yanaonekana kwenye ubapa wa juu wa jani la tunda bukini nyekundu na nyeupe. Kwa kawaida, malengelenge haya huwa ya kijani-manjano kwenye currant nyeusi. Maeneo yaliyobadilika rangi mara nyingi huzunguka tishu zilizoharibika. Kawaida, majani kwenye ncha za matawi yanaonekana yamejikunja au kuharibika umbo. Uharibifu mkubwa wa majani unaweza kutokea kutokana na uvamizi mkubwa wa vidukari. Vidukari wa rangi ya njano iliyofifia wanaweza kupatikana chini ya maeneo yenye malengelenge mwishoni mwa majira ya kuchipua hadi mwanzoni mwa majira ya joto. Umande wa asali unaweza pia kuwepo kwenye majani. Umande huu hatimae huchangia ukuaji wa vimelea vya ukungu (kuvu) wa majivu meusi. Kwa kawaida, vichaka bado vinaweza kutoa mazao ya kawaida licha ya dalili ndogo kwenye majani.
Wadudu wa asili wanaosaidia kudhibiti vidukari ni pamoja na wadudu vibibi – hawa wanaweza kuachiliwa kwenye shamba ikiwa mlipuko unatokea. Dawa za kupulizia zenye sabuni zinazotengenezwa kwa mafuta asili au mchanganyiko mwepesi wa sabuni za kuoshea vyombo zinatosha kudhibiti vidukari wa currant nyekundu. Vidukari pia wanaweza kuondolewa kwa kupuliziwa maji kwa nguvu kutoka kwenye mpira wa maji. Matumizi ya dawa zinazotengenezwa na mafuta asili yanaweza kutumika kuua mayai yanayoishi msimu wote wa baridi. Michanganyiko mingine ya kikaboni inayoua vidukari wanaoibuka ni pamoja na za kuua wadudu zinazotokana na pareto, na asidi za mafuta.
Daima zingatia mbinu jumuishi kwa kuchukua hatua za kuzuia pamoja na tiba za kibaiolojia ikiwa zinapatikana. Katika hali mbaya ya maambukizi, dawa za kuua wadudu za kupulizia zenye deltamethrin au lambda-cyhalothrin zinaweza kutumika kuua vidukari wanaoibuka. Usisubiri dalili za kuonekana ili kuchukua hatua, kwani inakuwa haina maana tena kupulizia dawa baada ya majani kujikunja. Usipulizie dawa kwenye mimea inayochanua maua ili kuepusha hatari kwa nyuki na wadudu wengine wa uchavushaji.
Uharibifu husababishwa na vidukari wa malenge lenge ya tunda bukini jekundu, na vidukari hawa wanafahamika kitaalamu kama Cryptomyzus ribis. Tishu za majani yaliyojikunja na yenye malengelenge mara nyingi huonekana zaidi kuliko vidukari wasio na mbawa na wenye rangi ya njano hafifu ambao hufyonza utomvu unaokuwa chini ya majani, ambayo huonekana mwishoni mwa majira ya kuchipua au mwanzoni mwa majira ya joto. Malengelenge na mabadiliko ya rangi husababishwa na kemikali zinazoingizwa na vidukari kwa kudunga majani wakati wa kuyala. Kufikia katikati ya majira ya joto, vidukari wenye mbawa huzaliwa na kuhamia kwa mimea mingine inayohifadhi vimelea. Kufikia majira ya vuli, vidukari hawa hurudi kwenye mmea wa currant, na hutaga mayai yanayoishi msimu wote wa baridi kwenye vitawi. Mayai huanguliwa msimu wa kuchipua na kuzalisha makoloni ya vidukari ambao huhamia kwenye upande wa chini wa majani. Vidukari wa malengelenge ya matunda bukini huathiri matunda bukini mekundu, meupe na meusi, pamoja na matunda mwitu jamii ya jostaberi. Kwa kuwa kwa kawaida mazao huwa hayathiriwi, hatua za kudhibiti zinapaswa kuchukuliwa tu katika hali mbaya sana ya maambukizi.