Pamba

Panzi Jasidi wa Majani ya Pamba

Amrasca biguttula

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Kutokea kwa rangi ya manjano na kukunjamana kwa majani kuelekea juu.
  • Kubadilika kwa rangi ya kahawia ikianzia kwenye kingo katika hatua za baadaye.
  • Kudondoka kwa majani yaliyokauka.
  • Ukuaji uliodumaa.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Pamba

Dalili

Majani yaliyoathirika hugeuka kuwa ya manjano kisha ya kahawia kuanzia kwenye kingo na kuenea hadi kwenye mshipa wa katikati. Majani huanza kuonyesha dalili za kukunjamana kabla ya kukauka kabisa na kudondoka. Matukio makali husababisha jeraha la “hopper burn” na kufa kwa majani, na hatimaye kusababisha udumavu wa wa mimea michanga. Uwezo wa kutoa matunda kwa mimea iliyoathirika katika hatua za baadaye za ukuaji huathirika sana na mara nyingi husababisha mavuno kidogo na ubora duni wa nyuzinyuzi za pamba.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Wadudu wawindaji wa jumla wanaowinda na kula panzi wa pamba ni pamoja na mbawakimia wa kijani wa kawaida (Chrysoperla carnea), spishi za jenasi Orius au Geocoris, spishi kadhaa za Coccinellids na buibui. Hakikisha unakuza idadi ya spishi tajwa na epuka matumizi makubwa ya dawa za kuua wadudu. Tumia Spinosad (0.35 ml/l) pale dalili za kwanza zinapotokea.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaolojia ikiwa yanapatikana. Michanganyiko ya dawa za kuua wadudu zinazotokana na cypermethrin (1 ml/l), sulfoxaflor, chlorpyrifos (2.5 ml/l), dimethoate, lambdacyhalothrin (1 ml/l) au chlorantraniliprole + lambda-cyhalothrin (0.5 ml/l) inaweza kutumika. Hata hivyo, dawa hizi zinaweza pia kuathiri wadudu wawindaji asili wanaowinda na kula panzi waharibifu na kwa hiyo zinapaswa kutumiwa tu katika hali mbaya na kwa wakati mwafaka. Matibabu ya mbegu kwa kutumia dawa za kuua wadudu yanaweza pia kusaidia kupunguza idadi ya panzi waharibifu kwenye mazao kwa siku 45-50.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na tunutu na wadudu kamili wa Amrasca. Wadudu hawa hunyonya utomvu wa mimea na kuingiza sumu za mate ambazo zina uwezo wa kuharibu tishu na kudhohofisha usanisinuru. Joto la wastani hadi la juu na unyevunyevu unaoanzia asilimia 21 hadi 31°C na asilimia 55 hadi 85 mtawalia, huchochea uwepo na shughuli za wadudu hawa. Joto la kiwango cha chini na upepo mkali huzuia shughuli za wahudu hawa.


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina za mbegu zinazostahimili au kuvumilia magonjwa (kuna aina kadhaa zinapatikana sokoni).
  • Kagua shamba mara kwa mara kugundua dalili za panzi wa pamba.
  • Dumisha matumizi ya mbolea kwa uwiano sahihi na hasa usitumie mbolea ya naitrojeni kupita kiasi.

Pakua Plantix