Colaspis hypochlora
Mdudu
Mbawakawa waliokomaa hula magugu mbalimbali, pamoja na majani machanga ambayo hayajafunuka, mashina, na mizizi ya migomba. Pia hula kwenye tunda/ndizi changa, na kutengeneza makovu na madoa kwenye ganda, madoa ambayo huiharibu na kuifanya ishindwe kuuzika. Makovu mengi hutokea chini (kitako) ya matunda, hii ikiwa ni kuonyesha ukweli kwamba mbawakawa walichagua maeneo yaliyohifadhiwa zaidi kwa ajili ya kula (kwa mfano, chini ya bract). Makovu kwa kiasi kikubwa yana umbo la yai na yanaweza kufananishwa na yale makovu ya matunda yanayoambukizwa na nyuki wasiong'ata wanaofahamika kama Melipona amalthea. Uharibifu huo unafanywa kuwa mbaya zaidi na uwepo wa vimelea nyemelezi kwenye tishu. Mabuu hula kwenye mizizi michanga, na kuweka vihandaki kwenye mizizi mikubwa na kula tishu zake. Utokeaji wa wadudu hawa kwa kawaida huwa juu wakati wa msimu wa mvua.
Hakuna matibabu ya kibaolojia yanayoweza kupatikana kwajili ya wadudu hawa hadi sasa. Njia bora ya kuzuia ili kuepuka kuenea kwake ni mpango mzuri wa upaliliaji wa magugu.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Udhibiti kwa kutumia madawa ya kemikali kwa kawaida haupendekezwi, kwa sababu uondoaji mzuri wa magugu, kwa mfano, unaweza kupunguza idadi kubwa ya wadudu ili kuepuka matumizi ya madawa ya kuulia wadudu. Nyunyizia dawa za kuua wadudu kwa mzunguko kutegemea na ukubwa wa tatizo la wadudu. Hata hivyo, matumizi ya madawa ya kuua wadudu yanapaswa kuepukwa isipokuwa tu kama mbawakawa wanasababisha hasara kubwa za kiuchumi.
Uharibifu huo unasababishwa na mbawakawa wa migomba aina ya Colaspis hypochlora. Mbawakawa wakubwa wana mbawa za mbele zenye rangi ya kahawia na safu za madoa madogo yanayokaa sambamba. Mbawakawa ni warukaji wazuri sana. Majike hutaga mayai ya rangi ya limau-njano, moja moja au kwa makundi yanayotofautiana kwa idadi kutoka 5 hadi 45. Utagaji wa mayai hufanyika kwenye vishimo/uvungu vilivyogugunwa (vilivyotafunwa) kwenye ala (sehemu ya jani iliyojifunga) ya majani karibu na eneo la juu la mmea au kwenye korongo/shimo la asili linaloonesha wazi mizizi. Baada ya siku 7 hadi 9, mabuu wapya walioanguliwa huanza kula mizizi michanga au kutoboa vihandaki kwenye tishu laini za ngozi ya mizizi na kuanza kuila. Mbawakawa wana miili myeupe, myembamba na yenye nywele nyingi, na kichwa kina rangi ya kaharabu (mithili ya rangi ya manjano). Pupa, wana rangi ya manjano chafu, ambayo hubadilika kuwa nyeusi kadiri anapokua mkubwa na kuwa tayari kujitokeza kama mbawakawa kamili.