Acrocercops syngramma
Mdudu
Dalili za awali za shambulio huonekana kama machimbo kwenye majani machanga. Lava hula tishu za majani huku wakiacha tabaka la ngozi la nje bila kuguswa. Mabaka meupe yenye malengelenge hatimae huonekana kwenye uso wa majani ambako sehemu kadhaa zilizochimbwa huungana. Uharibifu huonekana kama mashimo makubwa kwenye majani ya zamani na yaliyopevuka. Hii husababishwa na kukauka na kusambaratika kwa sehemu zilizochimbwa za jani.
Tumia nyigu wa vimelea kama vile Diglyphus isaea, ambaye hushambulia lava wa kidomozi, na kuwaua kabla hawajakua. Tumia mbolea za kikaboni ili kudumisha afya ya mimea. Zuia vidomozi wakubwa kutaga mayai kwenye majani kwa kutumia vifuniko vya safu vinavyoelea. Mitego inayonata yenye rangi ya njano au ya samawati inaweza kutumika kuwanasa vidomozi wanaotaga mayai. Udongo chini ya mimea iliyoathiriwa unapaswa kufunikwa na matandazo ya plastiki ili kuwazuia lava kufika ardhini na kukomaa. Dawa ya kunyunyizia yenye mkusanyiko wa mafuta ya Mwarobaini na cypermethrin huvuruga ukuaji na maendeleo ya wadudu waharibifu.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na tiba za kibaiolojia, ikiwa zinapatikana. Nyunyiza Monocrophos 36 WSC 0.05% (@ 0.5ml/lita). Dawa za kuua wadudu za mimea zinazofanya kazi kwa haraka zinapaswa kutumiwa tu kama suluhisho la mwisho.
Uharibifu husababishwa na lava wa kidomozi. Mayai yanatagwa kwenye majani machanga na kipepeo kamili mwenye rangi ya kijivu iliyo mithili ya fedha. Kabla ya kukomaa, lava huwa na rangi nyeupe hafifu na baadaye hubadilika kuwa rangi ya waridi (pinki) au kahawia nyekundu. Lava hudondokea kwenye udongo ili kukomaa na kuibuka baada ya siku 7-9. Mzunguko mzima wa maisha unaweza kutofautiana kati ya siku 20 hadi 40. Uharibifu huu hupunguza uwezo wa mimea kufanya usanisinuru, na hivyo kusababisha upotevu mkubwa kwenye uzalishaji kwa sababu majani hukauka na kudondoka.