Pistachio

Mbawakavu wa Mfistiki (Pistachio)

Chaetoptelius vestitus

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Uharibifu wa machipukizi na matawi, na kupelekea kunyauka na kufa.
  • Uwepo wa vijumba/vihandaki kwajili ya kuzaliana katika matawi na shina.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Pistachio

Pistachio

Dalili

Mbawakavu wakubwa huchimba vijumba/vihandaki kwa kula kupitia machipukizi na kuyaharibu, na kuhatarisha uundaji wa matunda. Vijumba vya kujihifadhi katika shina au matawi pia huvuruga mzunguko wa kawaida wa utomvu/majimaji, hivyo kuzuia maji na virutubishi kufikia matawi juu. Mbawakavu wakubwa wana rangi ya kahawia-nyeusi, urefu wa karibu milimita 2.5-3.5 na vifuniko vya mabawa vyeusi vyenye alama ya nywele ngumu. Mara nyingi lava ni weupe na kichwa cha kahawia. Ni mdudu mwenye kujifaidisha hushambulia hasa miti iliyodhoofika na hivyo kukausha matawi yaliyovunjika. Wakati wa msimu wa baridi, ili mradi joto liko chini ya +5 ° C, mbawakavu wa gome huacha kula. Katika hali nzuri, anaweza kuwa na madhara sana kwa miti ya pistachio

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Ili kudhibiti mende wa gome, ni muhimu kuwa na miti imara, yenye afya na kuhakikisha matumizi mfululizo ya hatua za kuzuia pamoja na mashamba ya jirani. Baadhi ya nyigu wa vimelea hushambulia mbawakawa huyu, kama vile mbawakawa kadhaa wawindaji na utitiri. Athari zao za udhibiti zimekadiriwa kuwa karibu 10% ya idadi ya wadudu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kuzuia na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Mdudu huyu hapatikani kwa udhibiti rahisi wa kemikali hata kama zikichanganywa na mafuta ya madini ambayo huwezesha kupenya kwa wadudu. Kwa hiyo, hatua za kuzuia ni muhimu ili kuepuka kuenea kwake. Zinapaswa kutumiwa na wakulima wote katika kanda ili wadudu wasiweze kuhama kutoka kwenye bustani zilizoathiriwa hadi zenye afya. Mbawakawa wa gome hushambulia hasa miti iliyodhoofika, hivyo ni muhimu kuhakikisha miti ina afya (kuweka mbolea, umwagiliaji, kupogoa, kudhibiti wadudu na magonjwa).

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu huo unasababishwa na mbawakavu Chaetoptelius vestitus, mshirika wa familia ya Scolytidae. Wadu wakubwa huibuka Aprili-Mei wakati joto linapoongezeka zaidi ya 25 ° C. Majike huruka hadi kwenye matawi machanga ya miti yenye afya ili kutoboa vihandaki vifupi kwenye sehemu ya mwisho au machipukizi ya maua, na hivyo kuyaharibu. Baadaye pia huanza kula shina na matawi machanga, ambayo hunyauka haraka sana kama matokeo ya uharibifu. Wakati wa majira ya joto na baridi mbawakavu hubumbwaa(kujituliza kama wamekufa) ndani ya matawi ya pistachio. Mwishoni mwa majira ya baridi, majike hutafuta matawi dhaifu au yaliyovunjika ambapo huchimba vijumba kwajili ya kuzaliana na kutaga takriban mayai 80-85.


Hatua za Kuzuia

  • Mwagilia maji kulingana na ratiba, hasa wakati wa kiangazi, ili kuepuka mfadhaiko wa ukame.
  • Pogoa na choma matawi makavu na dhaifu ambayo yanaweza kushambuliwa na wadudu.
  • Dumisha usafi wa bustani kwa kuondoa magugu na matawi yaliyokufa.
  • Kagua miti iliyo pogolewa kwa uwepo wa mbawakavu wa gome, lava wake, au vijumba vyake.
  • Mitego ya miti inaweza pia kuwekwa katika shamba lote ili kuvutia wadudu wakubwa kwenye matawi dhaifu, yaliyokauka na kisha kuyachukua na kuyachoma.

Pakua Plantix