Parlatoria ziziphi
Mdudu
Maambukizi ya Vidugamba Weusi yanajulikana kutokana na uwepo wa wadudu wadogo weusi wanaokula kwenye matawi, majani, na matunda. Katika maambukizi makubwa, vidugamba weusi wenye umbo mithili ya mstatili, ambao ni ngumu kuondolewa na vijidudu vyao vyeupe vinavyotambaa kiuhalisia hufunika matunda, majani, na matawi kwa kiasi kikubwa. Upungufu wa utomvu wa mmea husababisha kupungua kwa uimara wa mmea unaohifadhi wadudu na ukuaji wa madoa ya njano au michirizi kwenye maeneo ya kula. Ulaji wao unaua matawi na kunaweza kuathiri sana ukuaji wa matunda, mara nyingi husababisha kuharibika kwa umbile la matunda hayo. Hii inaweza kusababisha kuzeeka mapema kabla ya wakati, kudondoka kwa majani na matunda, na kupungua kwa wingi na ubora wa matunda. Spishi hizi zimekuwa mdudu muhimu zaidi wa mimea jamii ya machungwa.
Baadhi ya vimelea wa nyigu, ikiwa ni pamoja na Scutellista caerulea, Diversinervus elegans, na Metaphycus helvolus, pamoja na baadhi ya spishi za jenasi Aspidiotiphagus na Aphytis wanaweza kusaidia kudhibiti vidugamba weusi. Wadudu kama vile wadudu-kibibi wanaweza pia kuangamiza idadi ya vidugamba weusi katika mipangilio inayofaa. Mafuta ya kanola au viuatilifu vya kibaiolojia vinavyotokana na kuvu (ukungu) pia vinaweza kutumika kudhibiti vidugamba weusi. Mchanganyiko wa mafuta meupe (kwa mfano, uwiano wa sehemu 4 za mafuta ya mboga na sehemu moja ya sabuni ya kuoshea vyombo) unaweza kutumika kwa ufanisi dhidi ya vidugamba weusi huku kukiwa na athari ndogo kwa wadudu wengine muhimu kwa ikolojia.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu ya vidugamba weusi ni lazima yapangiliwe kwa wakati sahihi ili kudhibiti watambaaji/lava wa kizazi cha kwanza kati ya msimu wa baada ya kutoka maua na upuliziaji dawa wa kiangazi.
Dalili husababishwa na Vidugamba Weusi aina ya Parlatoria, ambapo mimea ya jamii ya machungwa ndiyo hifadhi yao. Ingawa majani ndio maeneo wanayopendelea kuishi, vidugamba hawa pia huishi na kula matunda pamoja na matawi. Hatua zote za ukuaji kwa vidugamba zipo kwa mwaka mzima, ikimaanisha kwamba mdudu huyu hukamilisha vizazi kadhaa vinavyopishana (ingiliana/pishanisha) kila mwaka, ikiwa ni kuanzia vizazi viwili hadi saba. Idadi hii pia inategemea sana maeneo yanakolimwa machungwa. Mzunguko kamili wa maisha unaweza kuchukua siku 30-40 huko Sicily katika hali nzuri, wakati nchini Tunisia huchukua siku 70-80 katika hali za joto na hadi siku 160 katika hali ya ubaridi.