Toxoptera aurantii
Mdudu
Hatua zote za ukuaji wa miti ya machungwa zinaweza kuathiriwa. Vidukari wana sehemu ndefu za mdomo zinazochoma ambazo hutumia kunyonya utomvu kwenye ncha za mashina na majani machanga, na hivyo kusababisha kuharibika kwa vitawi na kujipindapinda, kujisokota, au kujikunja kwa majani. Vidukari wanapokula kwenye floemu tamu ya mmea, wanatoa sukari ya ziada kama umande wa asali. Umande huu wa asali unapodondoka kwenye majani, majani hayo yanakuwa tayari kukaliwa na kuvu mithili ya masizi ambao hufanya majani kuwa meusi. Hali hii hupunguza usanisinuru na kuwa na athari kwa uimara wa mti na ubora wa matunda. Uharibifu kwa miti ya machungwa unaweza pia kutokana na maambukizi ya virusi vya tristeza, ambavyo hubebwa na vidukari.
Wadudu wanaokula vidukari ni pamoja na spishi nyingi za nzi waeleaji, mbawakimia, na wadudu-kibibi ambao wanaweza kushambulia vidukari katika hatua zote za ukuaji. Wadudu-kibibi wawili wanaotumika sana dhidi ya mdudu huyu ni wadudu kamili (waliokomaa/wakubwa) na lava wa wadudu-kibibi wasio na madoa wadudu-kibibi convergens. Baadhi ya nyigu-vidusia wanaweza pia kupatikana kwa ajili ya matunda jamii ya machungwa katika eneo la kupendezwa.Kuvu Neozygites fresensii inaweza kuwa kipimo muhimu kwa idadi ya vidukari wakati wa hali ya hewa ya unyevunyevu. Chungu wanaweza kuuawa kwa maji ya moto au kwa mchanganyiko wenye dawa asili ya pyrethrins. Mchanganyiko wa dawa za kuua wadudu unaweza pia kutumika dhidi ya vidukari, kwa mfano mchanganyiko unaotokana na sabuni, sabuni za kufulia/kuoshea vyombo, mafuta ya mwarobaini au pilipili.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na tiba za kibiolojia ikiwa zinapatikana. Dawa kadhaa za kuua kuvu/ukungu zinaweza kutumika kudhibiti vidukari lakini ufanisi wake unategemea matumizi kwa wakati sahihi, kwa mfano kabla majani hayajajikunja au kabla idadi ya vidukari haijakuwa kubwa sana. Bidhaa za kibiashara zenye mafuta ya petroli zinaweza kupuliziwa upande wa chini wa majani, ili ziwaguse vidukari moja kwa moja. Dawa zilitengenezwa kutokana na maua ya pareto pia zinaweza kuwa na ufanisi dhidi ya vidukari na chungu, lakini zinaweza pia kuwa na athari mbaya kwa maadui wa asili.
Dalili husababishwa na vidukari kamili (waliokua) pamoja na viwavi wa vidukari weusi wa machungwa waitwao Toxoptera aurantii. Mara nyingi huambukiza miti ya machungwa na mimea mingine pamoja na spishi zingine za vidukari inazohusiana nayo, T. citricida, wanaojulikana kama vidukari wa machungwa wa kahawia. Vidukari kamili wanapatikana katika maumbo mawili, ama wenye mbawa au wasio na mbawa. Vidukari wenye mbawa wanaweza kuruka umbali wa hadi kilomita 30 na huonekana wanapokuwa wengi sana au kunapokuwa na uhaba wa chakula. Wadudu hawa wana miili yenye rangi ya kahawia iliyofifia hadi nyeusi, na urefu wa takriban milimita 1.5. Vidukari weusi wa machungwa wana mzunguko rahisi wa maisha na kiwango cha juu cha uzazi ambacho kinaweza kusababisha maambukizi ya haraka na makubwa. Kiwango muafaka cha joto kwa ajili ya ukuaji, kuishi na kuzaliana ni kati ya 9.4 na 30.4 °C. Umande wa asali huvutia mchwa, ambao nao huwalinda vidukari dhidi ya wadudu wa asili wanaokula vidukari. Aidha, vidukari hawa wanachukuliwa kuwa ni wabebaji wa ugonjwa wa tristeza wa machungwa na batobato wa zuchini.