Brassicogethes aeneus
Mdudu
Dalili iliyo wazi zaidi ya mashambulizi ni uwepo wa mbawakavu weusi na wanaong'aa wakitembea kwenye maua ya mmea mwenyeji. Mashimo kwenye machipukizi huonesha mahali ambako mbawakavu wakubwa wamekula au kutaga mayai yao kwenye machipukizi. Uharibifu mkubwa kwa machipukizi unaweza kusababisha machipukizi kudondoka na kuacha vikonyo visivyo na matumba. Ulaji kwenye maua unaishia kwenye stameni zinazobeba chavua na dalili chache zinazoonekana zinajitokeza.
Utengenezaji wa Bacillus thuringiensis umetumika kwa mafanikio fulani dhidi ya B. aeneus.
Daima zingatia mbinu jumuishi kwa kutumia hatua za kinga pamoja na tiba za kibaiyolojia ikiwa zinapatikana. Mimea ya brokoli na kauliflawa inaweza kutumika kama mazao ya mtego kwa kupuliziwa dawa za kuua wadudu, kwa kawaida dawa ya deltamethrin. Baadhi ya majaribio yalionyesha kwamba karibu ulinzi kamili unaweza kupatikana, lakini hili linategemea uwezo wa kuzalisha zao la mtego linalotoa maua kabla ya zao kuu, jambo ambalo linaweza kuwa gumu kupangilia wakati. Dawa za kuua wadudu za pyrethroid zinaweza pia kutumika kudhibiti B. aeneus ikiwa hakuna matukio yanayofahamika kuhusu usugu wao dhidi ya kemikali hiyo. Hata hivyo, dawa za pyrethroid pia huathiri viumbe wanaokula wadudu. Fikiria kutumia neonicotinoids, indoxacarb au pymetrozine kama mbadala wa pyrethroids. Usipulize baada ya maua kuanza kuchanua.
Mbawakavu wakubwa hutokea katika msimu wa kuchipua baada ya kuishi kipindi cha baridi kali katika maeneo ya misitu na maeneo mengine ya kujificha ambayo hayalimwi. Wanaruka kwa nguvu wakati joto linapozidi 12-15°C, mara nyingi wakila chavua ya maua yoyote yaliyopo kabla ya kufika kwenye mimea yao ya kuzaliana. Mayai huwekwa kwenye vitumba vilivyo na urefu wa angalau mm 3. Lava hula chavua katika machipukizi, na huchukua siku 9-13 kukamilisha hatua mbili za lava. Lava aliyekomaa kikamilifu hatimae hudondoka ardhini, na kujizika mwenyewe kwenye udongo. Mbawakawa/mbawakavu wakubwa wapya hutokea baadaye na kula chavua kutoka kwa maua yoyote yaliyopo kabla ya kutafuta tena maeneo ya kuishi katika msimu mzima wa baridi kali. Usambazaji wa B. aeneus kwenye mazao kwa kawaida ni mgumu na hauna utaratibu maalum.