Mythimna separata
Mdudu
Dalili ni pamoja na uharibifu unaotokana na ulaji kwenye ncha za majani au kingo za majani, wakati mwingine huacha mshipa wa katikati pekee (skeletonization ya majani). Wakati wa mashambulizi makali, lava wakubwa wanaweza kuondoa majani yote na hata miche mizima kutoka kwenye kitako. Tabia ya M. separata pia ni kukatwa kwa kitako cha masuke, na yale ambayo yamesalia huinama tu au kuanguka. Lava wachanga wa kijani wenye mistari mgongoni huonekana kwenye mimea. Uharibifu mara nyingi huelekezwa kwenye sehemu moja ya shamba. Wakati wa milipuko mashamba mengi yanaweza kuathiriwa wakati huo huo lava huhama kwa makundi kati yao.
Baadhi ya aina kali za nyigu Cotesia ruficrus na Eupteromalus parnarae zimetekelezwa kwa mafanikio mashambani. Wadudu hawa hutaga mayai kwenye lava wa M. separata, na kuwaua polepole. Njia muhimu ya kitamaduni ni pamoja na kupandisha kiwango cha maji wakati idadi wadudu iko katika hatua ya pupa ili kuwazamisha. Mafuriko pia yanazuia kusambaaji kutoka mmea hadi mmea wa lava wa M. separata. Bata katika mashamba ya mpunga pia husaidia kudhibiti idadi ya wadudu.
Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kinga na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Ili kuzuia viwavi kuhamia shamba lingine, nyunyiza dawa ya cypermethrin kwenye mpaka wa mashamba yaliyoshambuliwa ili kuepuka kuhama kwa lava. Ikiwa kuna uvamizi mkubwa wa viwavi jeshi, dawa ya kemikali ni muhimu. Inashauriwa kunyunyiza cypermethrin @ 1 ml / 1 l ya maji. Wakati mzuri wa kunyunyizia dawa ni majira ya jioni.
Uharibifu huo husababishwa na lava wa viwavi wanaokata masikio/masuke ya mpunga, Mythimna separata. Wadudu waliokomaa wana mbawa za mbele za rangi ya kijivu-njano na rangi ya kijivu iliyokolea au nyekundu-njano na yenye madoa mengi meusi. Majike hutaga mayai ya mviringo, ya nyeupe-kijani hadi nyeupe kwenye majani, yakiwa wazi au yamefunikwa na utando mwembamba wenye weusi. Lava wachanga wa kijani ya nyasi wenye michirizi mgongoni huonekana mara moja kwenye mimea na kuanza kusababisha uharibifu. Vipindi vya ukame vinavyofuatiwa na mvua kubwa hupelekea maisha marefu ya wadudu waliokomaa, urefu wa kipindi cha utagaji na kuanguliwa kwa mayai. Mbolea ya naitrojeni huboresha ukuaji wa mimea na kusababisha ulaji zaidi na kuishi kwa lava. Wenyeji mbadala ni pamoja na, miongoni mwa wengi, shayiri, ngano, mahindi, oti, mtama, miwa, mianzi, pamba, viazi vitamu, tumbaku na aina za kabeji.