Scirtothrips dorsalis
Mdudu
Tunutu na wadudu kamili hula upande wa chini wa majani machanga. Wanakwaruza na kutoboa tishu na kunyonya utomvu unaotoka. Majani yaliyoshambuliwa huwa na madoa ya kahawia hafifu hadi rangi ya fedha na yanaweza kuonyesha dalili za kuharibika (kujikunja). Katika hali mbaya kuna uharibifu wa jumla wa umbo la majani na baadaye mmea kupukutisha majani mapema. Ulaji kwenye maua huonekana kama michirizi ya petali na unaweza kusababisha kukauka na kudondoka. Magaga, madoa na uharibifu wa matunda hupunguza thamani ya soko la matunda. Ingawa uvamizi hutokea mwaka mzima, huongezeka zaidi wakati wa miezi ya ukame na kwenye udongo wenye mbolea nyingi ya naitrojeni.
Mawakala mbalimbali wa udhibiti wa kibayolojia kama vile kunguni wadogo haramia wa jenasi Orius, na utitiri wa phytoseiid Neoseiulus cucumeris na Amblyseius swirskii wameripotiwa kutoa udhibiti mzuri wa vithiripi kwenye komamanga. Utitiri wawindaji kama vile Euseius sojaensis, E. hibisci na E. tularensis pia wametumiwa kwa ufanisi kudhibiti idadi ya vithiripi kwenye mimea mbadala kama vile pilipili na zabibu. Sambaza mwani kuzunguka kitako/shina la mmea na majani ya mimea ili kupunguza vithiripi na lava wao (jioni). Paka mafuta ya mwarobaini, spinetoram, au spinosad kwenye pande zote za majani na kuzunguka shina la mmea.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kunyunyuzia za majani zenye malathion zinapendekezwa kwa udhibiti wa vithiripi. Matumizi ya viuatilifu vingine pia yana ufanisi katika kupunguza idadi ya S. dorsalis. Kwa mfano, matumizi ya abamectin yanajulikana kuwa na ufanisi dhidi ya vithiripi wa matango kwa ujumla.
Dalili husababishwa na aina mbili za vithiripi, Scirtothrips dorsalis na Rhipphorothrips cruentatus. Scirtothrips dorsalis wakubwa wana rangi ya jano ya majani makavu. Majike hutaga takribani mayai 50 yenye umbo la maharagwe ya kijivu-nyeupe, kwa kawaida ndani ya majani machanga na vichipukizi. Kadiri idadi yao inavyoongezeka, huhamia pia kwenye uso wa majani yaliyokomaa. Kipindi cha kuatamia ni siku 3-8. Tunutu wapya walioanguliwa ni wadogo sana, na mwili mwekundu ambao baadaye hugeuka njano-kahawia. Tunutu wanapoingia kwenye mchakato wa metamofosisi huanguka kutoka kwenye mmea na kisha kukamilisha maendeleo yao katika udongo ulio legea au uchafu wa majani chini ya shina la mmea husika. Kipindi cha kuwa pupa huchukua siku 2-5. Wadudu kamili wa R. cruentatus ni wadogo, wembamba, wenye mwili laini na wenye mbawa zenye tarazo/tarizi sana, kahawia nyeusi na mbawa za njano na wana urefu wa 1.4mm.