Stephanitis typica
Mdudu
Maambukizi yanaonekana kwenye majani, hata kwa mbali. Mbawakimia wakubwa na tunutu wapo upande wa chini wa jani, ambapo wanaishi katika makoloni/makundi na hula kwenye majani. Mara nyingi, wadudu hula kwenye utomvu wa majani karibu na mshipa wa kati. Uharibifu unaotokana na ulaji huonekana kama vidoa vidogo vyeupe, vilivyobadilika rangi kwenye upande wa juu wa jani. Vinyesi vyeusi vya wadudu huachwa kwenye upande wa chini wa jani. Maeneo yaliyokaliwa na wadudu yanageuka kuwa ya manjano hadi kahawia baada ya muda na kukauka. Miti ina ukuaji uliodumaa na inaonekana kuugua.
Spishi za wadudu wanaokula wadudu wengine kama vile Stethoconus praefectus wanaweza kupunguza uvamizi ikiwa watatumika katika mbinu jumuishi. Mchanganyiko wa mafuta ya mwarobaini na kitunguu saumu (2%) unaweza kutumika kama kinyunyizio cha majani ili kudhibiti shambulio hilo.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia. Matumizi ya dawa za kuua wadudu ni njia ya kawaida ya kupambana na ugonjwa huu. Bidhaa zilizo na dimethoate zinaweza kutumika kama dawa ya kunyunyuzia majani. Hizi zinapaswa kunyunyuziwa hasa kwenye upande wa chini wa majani ili upate kufikiwa na dawa hii.
Wadudu wakubwa wana rangi ya manjano hadi nyeupe na ukubwa wa milimita 4 na mbawa zinazopitisha mwanga/zinazong'aa, zenye taraza mithili ya kimia/lesi. Mbawakavu majike hutaga takribani mayai 30 kwenye upande wa chini wa jani. Baada ya takriban siku 12 tunutu wa manjano huanguliwa. Hatua hii ya ukuaji huchukua takribani siku 13. Kwa sasa, hakuna maelezo ya kina yanayopatikana kuhusu hasara ya mavuno kutokana na kushambuliwa na Mbawakimia wa Migomba. Hadi sasa, hakuna ripoti kuhusu uharibifu mkubwa kwenye migomba unaosababishwa na wadudu hawa.