Phthorimaea operculella
Mdudu
Mdudu huyu anaweza kula aina mbalimbali za mazao ya jamii ya solanaceous lakini viazi hupendelewa. Lava hushambulia majani ya viazi, mashina, vikonyo na mizizi ( shambani au kwenye hifadhi). Wanakula tishu za ndani za jani bila kugusa ngozi, na kutengeneza malengelenge yenye uwazi. Mashina yanaweza kudhoofika au kuvunjika, na kusababisha kifo cha mmea. Lava huingia kwenye kiazi kupitia jicho na kutengeneza vihandaki vyembamba sambamba na uso au kuchimba vijumba visivyo na mpangilio kwenye mwili. Vinyesi vya lava vinaonekana kwenye sehemu za kuingilia ambazo ni wazi kwa magonjwa ya fangasi na bakteria.
Viziduo vya maganda ya chungwa, na aina ya Pithuranthos tortosus au Iphiona scabra, kati ya mimea mingine mingi, ilipunguza uzazi wa nondo. Nyigu wa vimelea wa spishi za Bracon gelechiae, Copidosoma koehleri au Trichogramma walipunguza idadi ya wadudu kwa kiasi kikubwa. Wawindaji ni pamoja na mchwa na mdudu kobe. Matumizi ya aidha granulovirus au Bacillus thuringiensis yanaweza kusababisha vifo vya 80% ndani ya wiki mbili. Katika baadhi ya nchi, uharibifu wakati wa kuhifadhi unaweza kupunguzwa kwa kufunika magunia na majani ya mikaratusi au Lantana.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Viua wadudu vya kundi la organophosphates vinaweza kunyunyiziwa kwenye majani. Pyrethroids inaweza kutumika kwa mbegu kama dawa ya kuzuia mashambulizi ya lava.
Nondo wakubwa wana mwili ulionyooka wa kijivu wenye antena zilizopanuka, mbawa za mbele nyembamba za kahawia zilizotawanyika na madoa meusi, na mbawa za nyuma za rangi ya kijivu nyepesi na pindo refu. Mara nyingi ni wadudu wa usiku na wanavutiwa na mwanga. Mayai hutagwa moja moja au kwa makundi kwenye majani au kwenye machipukizi yaliyo wazi kwenye udongo mkavu. Wanashindwa kuanguliwa wanapowekwa kwenye joto chini ya 4°C kwa muda mrefu. Lava wana vichwa vya kahawia iliyokolea na miili ya rangi ya hudhurungi hadi waridi. Wanatoboa kwenye vikonyo, mashina mchanga au mishipa ya majani na baadaye kwenye mizizi, na kutengeneza vijumba visivyo na umbo maalumu. 25°C ndio halijoto bora zaidi kwa mzunguko wa maisha yao lakini uvumilivu ni kati ya 15 na 40°C. Nyufa katika udongo mkavu husaidia maisha ya lava.