Mbiringanya

Mbawakimia wa Bilinganya

Gargaphia solani

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Vinyesi vya kahawia kwenye sehemu ya chini ya majani.
  • Mabaka yaliyobadilika rangi kwenye majani.
  • Umanjano na kujikunja kwa majani.
  • Wadudu wadogo, wenye rangi ya kahawia iliyofifia na nyeupe.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mbiringanya

Dalili

Muda muhimu ni mwanzoni mwa majira ya kuchipua wakati mbegu za bilinganya bado ziko katika hatua ya miche. Tunutu (wadudu wadogo) wanakula upande wa chini wa majani kwa vikundi, wakiyafunika majani hayo kwa kinyesi cha rangi ya kahawia. Ulaji wa majani unasababisha mabaka ya duara yaliyobadilika rangi yanayoonekana wazi upande wa juu wa majani. Kuongezeka kwa uharibifu kunasababisha majani kubadilika rangi na kuwa ya manjano na hatimaye kunyauka na kujikunja. Maambukizi makali yanaweza kuua mimea yote au kuidhoofisha kiasi kwamba matunda yanashindwa kukua.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hifadhi maadui wa asili wa wadudu lesi wa bilinganya ikiwa ni pamoja na wadudu-kibibi, na buibui. Sabuni za kuua wadudu, pyrethrins na mafuta ya mwarobaini yanaweza kupuliziwa kwenye sehemu ya chini ya majani.

Udhibiti wa Kemikali

Kila wakati fikiria mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiyolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuua wadudu zenye upeo/wigo mpana na zinazotokana na maua ya pareto zinaweza kutumika kama dawa ya kupulizia majani, lakini zinapaswa kutumika kwa uangalifu kwani zinaweza kuathiri wadudu wa manufaa.

Ni nini kilisababisha?

Wadudu Lesi wakubwa wa bilinganya wana rangi ya kahawia nyepesi na nyeupe, wakiwa na vishipa angavu vya kijani, mithili ya kimia/lesi kwenye mbawa. Wanakaribia 4 mm kwa urefu na huishi kwenye mabaki ya mimea, wakisubiri hali za hewa nzuri ili kuibuka na kutaga mayai. Mayai ni ya kijani hafifu na yaliyogandishwa kwa makundi upande wa chini wa majani. Tunutu (Nymphs) hawana mbawa, wana rangi ya manjano na doa jeusi kwenye ncha ya tumbo. Tunutu na wadudu wakubwa wote wanaharibu majani, lakini wakati tunutu wanakula kwa sehemu moja, wadudu Lesi wakubwa huruka kwenda mimea mingine na kusambaza uharibifu kwenye mashamba hayo. Upotevu wa mavuno kwa kawaida huwa mdogo, lakini katika baadhi ya mazingira maalumu, upotevu unaweza kuwa mkubwa. Mbali na bilinganya, mimea mbadala inayohifadhi wadudu Lesi ni pamoja na viazi, alizeti, sage, pamba, mtunguja, na magugu ya horsenettle.


Hatua za Kuzuia

  • Fuatilia mimea kwa ukaribu ili kugundua ishara za uwepo wa mdudu huyu.
  • Ondoa wadudu kwa mkono au majani yaliyosambaa wadudu.
  • Ondoa mimea iliyoota yenyewe au mimea mbadala inayohifadhi wadudu kama vile magugu ya horsenettle na mtunguja.
  • Dhibiti matumizi ya dawa za kuua wadudu ili kuto athiri idadi ya wadudu wa manufaa(wanaokula wadudu waharibifu).
  • Ondoa mabaki ya mazao na magugu ili kuondoa maeneo ya wadudu kuishi katika msimu wa baridi.

Pakua Plantix