Mpunga

Panzi wa Kijani wa Mpunga

Nephotettix spp.

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Waenezaji wa ugonjwa wa tungro.
  • Kubadilika rangi kwa ncha za majani.
  • Kupungua kwa idadi ya machipukizi.
  • Ukuaji uliodumaa.
  • Panzi wa majani wenye rangi ya kijani iliyo fifia walio au wasio na alama nyeusi.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Mpunga

Dalili

Panzi wa Kijani warukao kwenye majani ndio wanaojulikana zaidi katika mashamba ya mpunga na husambaza ugonjwa wa virusi vya tungro. Virusi hivyo husababisha kubadilika rangi kwa ncha za majani, kupungua kwa idadi ya vipando/machipukizi, mimea iliyodumaa na isiyo na nguvu, na katika hali mbaya zaidi mmea kunyauka. Ili kutofautisha dalili za mazao yaliyoambukizwa na tungro na upungufu wa naitrojeni au sumu za chuma, angalia uwepo wa wadudu: mayai meupe au rangi ya njano ndani ya vifuko-jani au mshipa wa katikati; tunutu wa njano au rangi ya kijani hafifu wenye au wasio na alama nyeusi; wadudu kamili wenye rangi ya kijani hafifu wenye alama nyeusi au wasio na alama na wenye mwendo wa kimshazari.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Udhibiti wa kibiolojia ni pamoja na nyigu wadogo (hushambulia mayai), mende wa mirid; strepsipterans, nzi pipunculid, na sota (hushambulia vyote wadudu wakubwa na tunutu), kunguni wa majini, wadudu wa nabid, nzi wa empid, damselflies, kerengende, na buibui au vimelea vya magonjwa ya ukungu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa kadhaa za kuua wadudu zinapatikana sokoni dhidi ya wadudu hawa. Wasiliana na muuzaji wako wa karibu ni suluhisho gani linalofaa zaidi kwa hali halisi iliyopo shambani. Matibabu mbadala ya buprofezin au pymetrozine ni muhimu. Epuka matumizi ya kemikali kama vile chlorpyriphos, lamda cyhalothrin au michanganyiko mingine sanisi ya parethroidi ambayo wadudu wana uwezo wa kustahimili.

Ni nini kilisababisha?

Panzi wa Kijani warukao kwenye majani ni kawaida katika mazingira ya ardhi oevu yenye mvua na umwagiliaji. Hawapatikani/hawajaenea katika mpunga wa nyanda za juu. Tunutu na wadudu wakubwa hula kwenye upande wa nyuma wa majani badala ya kwenye vifuko-jani ya majani na majani ya kati. Pia wanapendelea mimea ya mpunga ambayo imerutubishwa kwa kiasi kikubwa cha naitrojeni. Kwa kawaida sio wadudu wa kuhofia, isipokuwa wakati wa kusambaza RTV.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina zinazostahimili wadudu na ugonjwa wa tungro (mfano: CR-1009).
  • Punguza idadi ya mazao ya mpunga hadi mawili kwa mwaka.
  • Sawazisha uanzishwaji wa mazao katika mashamba yote.
  • Panda mapema ndani ya kipindi fulani cha upanzi, haswa wakati wa kiangazi.
  • Fanya mzunguko wa mazao na zao lisilo la mpunga wakati wa kiangazi.
  • Mitego ya mwanga inaweza kutumika kuonyesha au kupunguza idadi.
  • Weka naitrojeni kama inavyopendekezwa.
  • Dhibiti magugu shambani na kando ya shamba ili kupunguza wenyeji mbadala.

Pakua Plantix